Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mtangazaji Julius Nyaisanga amefariki Dunia mkoani Morogoro

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mtangazaji Julius Nyaisanga amefariki Dunia mkoani Morogoro

Taarifa za kushtua katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na habari za kifo cha Mtangazaji mkongwe nchini Tanzania, Julius Nyaisanga, aliyekuwa mfanyakazi wa Abood Media mjini Morogoro.
 Julius Nyaisanga

 Kaimu Meneja wa Abood Media Abeid Dogoli ameithibitishia blog hii kwamba ni kweli mtangazaji wa siku nyingi Tanzania Julius Nyaisanga amefariki dunia leo asubuhi.

Amesema Nyaisanga alipelekwa hospitali ya Mazimbu Morogoro jana saa nane mchana kutokana na kusumbuliwa na Kisukari pamoja na presha ambapo asubuhi ya leo October 20 2013 ndio akafariki dunia akiwa na umri wa miaka 53.

Mara yake ya mwisho kuingia ofisini ilikua juzi japo alikua ameanza likizo toka October 12 ambapo huu ulikua ni mwaka wake wa tatu toka ameanza kufanya kazi na Abood Media ya Morogoro kama Meneja wa kituo.

 Katikati ni Julius Nyaisanga akiwa na wadau wengine wa habari. Kushoto ni Abubakar Lyiongo na kulia ni Othman Michuzi.
 
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger