Edo Kumwembe: Sikuwa na mkataba Coastal Union
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSEMAJI wa zamani wa Coastal Union,
Edo Kumwembe, amesema kwamba hakuwa na mkataba wowote ndani ya timu hiyo yenye
maskani yake jijini Tanga, badala yake alikuwa akifanya kazi kwa kujitolea kama
mdau wa mpira wa miguu.
Kumwembe aliyasema hayo siku chache baada ya kudaiwa kuwa amemaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo na hakuna juhudi za kuongeza ili aendelee na kibarua chake.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Kumwembe ambaye pia ni mchambuzi wa mambo ya soka, alisema kuwa lolote
linalotokea ndani ya timu hiyo hawezi kulalamika kwakuwa tangu mwanzo hakuwa na
mkataba wowote.
Alisema jambo hilo linamfanya aone
kuwa hana anachoharibikiwa katika suala hilo, ambalo habari zinazotolewa katika
vyombo vya habari zinasema Kumwembe na kocha wa Coastal Union, Hemed Morocco
mikataba yao imekwisha.
“Kama unazungumzia kocha wa Coastal
Union sawa, ila kwa upande wangu sikuwa na mkataba wa kuwa msemaji wa timu hiyo
yenye maskani yake jijini Tanga kwa wagosi wa kaya,” alisema.
Aidha, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
ya Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Albert Clement Peter , maarufu kama ‘Mkubwa
wa Kazi’ alikanusha vikali taarifa zilizosambazwa na baadhi vyombo vya habari
kuwa wamemfukuza kocha wao Morocco.
“Hatujamfukuza kocha huyo kama
ilivyoripotiwa bali mkataba wake wa kuendelea kuinoa timu hiyo umekwisha hivyo tutaandalia
hatima yake, huku kwa sasa akiwa Bukoba kwa ajili ya kukipiga na Kagera Sugar
ya mjini humo,” alisema.
Kwa mujibu wa Peter, uongozi unakaa
kuangalia namna gani ya kuendelea na kocha huyo au wamuache, ila si kweli kuwa
tayari ameshaondolewa kikosini.
Post a Comment