RAIS
wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela amerejea nyumbani kwake
mjini Johannesburg kimya kimya baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria
kwa muda mrefu.
Mandela mwenye umri wa miaka 95 alilazwa hospitali tangu Juni 8 mwaka huu baada ya kupata maambukizi katika map
afu.
Hali ya afya yake wiki iliyopita ilitajwa kuwa ‘mbaya lakini imara’ na haikutolewa taarifa tena kuhusiana na afya yake.
Maambukizi
ya ugonjwa wake yanasemekana kuhusishwa na kipindi cha karibu miongo
mitatu aliyokaa gerezani baada ya kufungwa kutokana na harakati zake za
kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
Post a Comment