DAYNA ADAI DIAMOND KAMUIBIA WIMBO WAKE WA MY NUMBER ONE.
Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro
alisema “Kukweli ni nimekwazika sana pia imeniuma,kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye.Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata,hivyo nikarekodi demo,nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba.
Baada ya muda ya nikamtafuta tena
vipi ili tufanye kabisa ile nyimbo,ndipo akaanza kusema yupo bize
nisubiri lakini.Lakini nashangaa sasa hivi nakisikia tena ile nyimbo
ameeimba yeye tena alafu kibaya zaidi ametumia beat ile ile pia na
mashairi yale yale.
Kiukweli alichokifanya sio kitu
kizuri,kwani watu wote tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi
maslahi yake.Na usiku wa jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya
wimbo huo.
Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana,nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya.
Post a Comment