KINANA AWASILI TANGA MJINI NA KUPOKEWA KWA SHANGWE.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akivuka na kivuko cha MV.Pangani kuelekea Wilaya ya Tanga mjini
ambapo anatazamiwa kukagua miradi mbali mbali na kushiriki ujenzi wa
maendeleo,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
(kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Pangani Ndugu Hamis Mnegero.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Pangani baada ya kuvuka na MV.Pangani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumuaga wakati akielekea Tanga mjni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kigombe ,Pangani ambapo aliwaeleza lazima kuwa makini katika kuchagua viongozi wa kijiji kwani wengi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi kiholela na kusababisha matatizo makubwa ya ardhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga mjini Mh.Omari Nundu wakati wa mapokezi katika kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini.
Wananchi wa kata ya Marungu wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata yao
Wasanii wa Tanga All Star wakionyesha ujuzi wa kuimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Marungu
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60 wa kata ya Marungu kutoka upinzani wamejiunga CCM .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60
Bibi Saumu Ngoma mama mzazi wa Diwani wa kata ya Marungu Ndugu Bakari Mambeya akirudisha kadi ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga na CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuezeka ofisi ya CCM kata ya Marungu.
Wazee wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wakiwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alishiriki kutoa kadi za mfuko wa afya ya jamii na kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wilaya ya Tangamjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Machui katika
kata ya Tangasisi
Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na
Wazee waasisi wa CCM Tanga mjini kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya
CCM wilaya ya Tanga mjini.
Mzee Athumani Makalo (wa kwanza kulia)
akiwa na wazee waasisi ndani ya ukumbi wa mkutano Halmashauri Kuu
ya CCM wilaya ya Tanga mjini.
Post a Comment