PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MFUKO
wa pensheni wa PPF umesema utawafikisha mahakamani waajiri ambao
hawapeleki michango kwa wakati kwani hali hiyo inasababisha usumbufu kwa
wateja wao.
Kauli
hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa Kanda ya Kinondoni, Tanga na
Pwani, Zahara Kayugwa wakati wa semina ya waajiri wa sekta mbalimbali
jijini hapa.
Alisema hatua hiyo inaweza kusaidia waajiri kufikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
“Kwa
kweli inatubidi tuchukue hatua, kwa sababu unakuta mfanyakazi anakuja
kudai mafao halafu mwajiri amechangia asilimia tano tu, sasa wateja
wanatuona kama sisi ni wababaishaji… hatutawavumilia tena," alisema
Kayugwa.
Aidha,
akifungua semina hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Salim Chima, alisema
Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii
nchini, hasa katika suala zima la kukuza na kuimarisha uchumi.
Post a Comment