ANCELOTTI AMENENA MAN CITY ITALAMBA DUME IKIMSAJILI LAMPARD
BOSI wa
Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini Manchester City itakuwa imelamba
dume kama itamsajili kiungo mkongwe Frank Lampard ambaye yuko mbioni
kujiunga Etihad kwa mkopo.
Kiungo
huyo mwenye miaka 36 aliachwa na Chelsea majira haya ya kiangazi mwaka
huu baada ya mkataba wake kumalizika na alisaini mkataba wa miaka miwili
na New York City FC mwezi juni mwaka huu.
Manchester City na New York Yankees wote wana hisa za umiliki wa New York.
Post a Comment