Kidau kushoto akiwa na raia wa Msumbiji aliyenunua jezi ya Yanga SC mjini Beira
Na Mahmoud Zubeiry, MAPUTO MJUMBE
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred
Kidau leo ameshuhudia namna klabu ya Yanga SC inavyohujumiwa nchini
Msumbiji. Asubuhi
ya leo, Kidau ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF akiwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo, nchini hapa alikutana kijana
mmoja akiwa amevalia jezi Yanga ambayo amenunua kwa watu wanaouza bila
idhini ya klabu hiyo. Kidau
alifika Uwanja wa Ndege kuwapokea washambuliaji Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC waliokuja kujiunga na Taifa Stars
kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Msumbiji kesho
Kijana
huyo raia wa Msumbiji, Magnum alisema kwamba jezi hiyo aliinunua Beira
na anafahamu kwamba Yanga SC ni timu ya Tanzania, lakini haijui. “Nimependa jezi nzuri, rangi nzuri nikanunua,”alisema kijana huyo ambaye alifika uwanja wa ndege kupata huduma za kibenki. Alisema
amenunua jezi hiyo kwa thamani ambayo ni sawa na fedha za Tanzania Sh.
15,000 na kwamba watu wengine pia wananunua kwa wingi na kuvaa jezi hizo
nchini Msumbiji. Kidau
alisema kwamba Yanga SC na watani wao Simba SC wanapoteza fedha nyingi
kutokana na kupuuza bishara ya jezi na bidhaa nyingine zenye nembo zao. “Sasa
watu ambao wanajua kama hii ni bishara nzuri, ndiyo wanajipatia fedha
nyingi kirahisi namna hii, hii ni biashara kubwa sana, klabu nyingi
Ulaya zinanufaika mno kwa biashara hii,”alisema kiungo wa zamani wa
Milambo ya Tabora, Simba SC na timu ya Taifa, Taifa Stars. Pamoja
na ukweli huo kwamba jezi za timu ni biashara inayoziingizia fedha
nyingi hata klabu kubwa Ulaya, lakini bado viongozi wa Yanga SC
hawajaonyesha kutaka kutumia fursa hiyo kuinufaisha klabu yao kiuchumi. Jezi
za Yanga pamoja na mahasimu wao, Simba SC zinapatikana karibu Afrika
Mashariki yote na nchi nyingine jirani ikiwemo Msumbiji. Wapembuzi
yakinifu wa masuala ya biashara hiyo wanaamini, kwa mwaka Simba na
Yanga zinakosa si chini ya Sh. Milioni 500 kila klabu kwa kupuuza
biashara ya jezi pekee.
Post a Comment