Ghala lenye dawa zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda limekamatwa Mwanza.
Maofisa
zaidi ya 30 kutoka mamlaka ya chakula na dawa na baraza la Famasi
Tanzania wamekamata ghala lenye dawa za serikali,zilizopigwa marufuku na
zilizokwisha muda wake wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni 97
zikiwa zinamilikiwa na mfanyabiashara wa jijini mwanza CHARLES MBUSIRO
kinyume cha sheria.
Ghala
hilo lililopo eneo la ilemela jijini mwanza limekutwa likiwa limesheheni
zaidi ya 120 za dawa ambazo ni sawa na tani 42 zikiwemo dawa za
serikali za Kenya na Uganda, dawa za misaada, dawa zilizopigwa marufuku
nchini kama vile klorokwini ya sindano, amodiaquine na gripe water -dawa
nyingine zilizokutwa ndani ya ghala hilo na kwenye duka lake la dawa
lililopo Natta barabara ya nyerere ni pamoja na ambazo hazijasajiliwa na
TFDA na azisizoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya dawa.
Meneja wa
usalama wa dawa wa TFDA Kissa Mwamwitwa ndiye aliyeongoza zoezi hilo
liliendeshwa chini ya usimamizi mkali wa askari polisi wenye silaha za
moto.
Baadhi ya
maofisa wanaotekeleza operesheni hiyo, wakiwemo wanasheria kutoka TFDA
na baraza la famasi tanzania pamoja na meneja wa mamlaka hiyo kanda ya
kati Florent Kyombo wakizungumzia tukio hilo wamesema taratibu za
kisheria zinafanyika ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa wa kahasa ilemela Richard Peter alikuwa shuhuda
wakati maofisa hao wa TFDA, baraza la famasi tanzania na askari polisi
walipokuwa wakitekeleza zoezi hilo kwenye ghala la dawa ambalo
linasemekana bado halijasajiliwa na TFDA huku mmliki wake charles
mbusiro akitoroka kwa kuruka ukuta na kutokomea kusikojulikana.(KILONGE)
Post a Comment