Featured Post Today
print this page
Latest Post

Ajali ya treni mkoani Dodoma jana

Ajali ya treni mkoani Dodoma jana

Treni iliyopata ajali wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma jana baada ya kusombwa na maji ikionekana pichani.
0 comments

Robert Mugabe kuususia mkutano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya endapo mkewe hataalikwa.

Robert Mugabe kuususia mkutano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya endapo mkewe hataalikwa.

Serikali ya Zimbabwe imeeleza kuwa rais Robert Mugabe ataususia mkutano uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa April kati ya Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU) endapo mkewe Grace hataalikwa.

Mkutano huo utafanyika Brussels, Ubeligiji (katika bara la Ulaya) ikizingatiwa kuwa mwaka 2002 Umoja wa Ulaya uliwawekea vizuizi Robert Mugabe na mkewe Grace kutozitembelea nchi za bara la Ulaya.
Mugabe ambaye ni makamo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) amepewa mualiko wa kuhudhuria mkutano huo lakini mkewe hakupewa mualiko huo.
Balozi wa EU nchini Zimbwabwe, Aldo Dell’Ariccia alieleza wiki iliyopita kuwa Umoja huo wa Ulaya unawaalika kwenye mkutano watu ambao wana kazi ya kufanya kwenye mkutano huo na kwamba program za kikao hicho hazihusishi wana ndoa.
Kauli ya balozi huyo ilionekana kumkera Mugabe na msemaji wake akarudisha mashambulizi kwa mshangao.
“Ni kitu cha kushangaza kwamba EU haikutoa mualiko kwa First Lady. Kitu ambacho Mungu amekiweka pamoja EU inataka kukitenga. Hivi wanatarajia rais aiheshimu EU na kuikosea heshima ndoa yake mwenyewe?” alikaririwa msemaji wa Mugabe, George Charamba.
Mke wa Mugabe alikuwa akikosolewa kuwa hutumia pesa nyingi kufanya manunuzi ya anasa kila anapolitembelea bara la Ulaya.
0 comments

Tuhuma nzito bungeni,ni za rushwa dhidi ya Waziri Mkuu Pinda.

Tuhuma nzito bungeni,ni za rushwa dhidi ya Waziri Mkuu Pinda.

Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la Katiba baada ya mjumbe Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kuwa waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo, huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.
Hoja ilipoanzia
Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana (Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani “walilia” sana kuwa Bunge la Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:“…Sasa kuna wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki.”
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
“Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
“Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi,” alisema Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Credit:Mwananchi.
0 comments

Timu ya uendeshaji wa huduma za afya wilayani Korogwe, mkoani Tanga

Timu ya uendeshaji wa huduma za afya wilayani Korogwe, mkoani Tanga

Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika jana Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kufungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (Kulia) akiongea wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (Katikati) katika ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (katikati) akifungua kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika mfumo wa afya ya Jamii mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga.
 Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
 Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini. 

 Mwenyekiti wa Kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Korogwe, Tanga (CHMT), Bw. Salim Bori (Kushoto) akijadili jambo wakati wa kikao cha majadiliano. Pembeni ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Bima ya Afya, Singida Bw. Issaya Shekifu akiwapa uzoefu jinsi wao walivyofanikiwa kwenye mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya CHF kwenda kwenye TIKA na Jinsi CHF inavyofanya vizuri wilayani Iramba kwa kauli mbiu ya "Kuku mmoja CHF na matibabu mwaka mzima.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (katikati) akijadiliana jambo na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia). Picha zote kwa hisani ya Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
0 comments

KAMATI YA UCHUMI NA FEDHA YA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE, TANGA YAPITISHA MPANGO WA TIBA KWA KADI (TIKA)

KAMATI YA UCHUMI NA FEDHA YA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE, TANGA YAPITISHA MPANGO WA TIBA KWA KADI (TIKA)

Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera akiendesha kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo Machi 27, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba (kushoto), anayefuatia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale (kulia) na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo Machi 27, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokata Jerry Mwakanyamale (kulia), Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri ya Mji Korogwe, Tanga wajadiliana jambo wakati wa kikao.
Diwani wa Kata ya Kwamdolwa, Mheshimiwa Hillary Ngonyani akijadili jambo.
Mchumi wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Bw. Kikonge Jeremiah akitoa tathimini zake juu ya matumizi ya Tiba Kwa Kadi (TIKA) kwa wananchi wa halmashauri yao.
Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi akitoa mwongozo na mtazamo wake katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA).
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (wa kwanza kulia) kitoa ufafanuzi wa vifungo vya sheria katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Afisa Muuguzi Kitengo Cha Afya ya Akili, Ayubu Mwakalila nae hakuwa nyuma kutoa mtazamo wake juu ya mada iliyokuwa ikijadiliwa. Picha zoe na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
0 comments

RC GALLAWA-VIONGOZI KUWENI MSTARI WA MBELE KUWAHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII MIJINI(TIKA)

RC GALLAWA-VIONGOZI KUWENI MSTARI WA MBELE KUWAHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII MIJINI(TIKA)

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIFUNGUA MKUTANO WA SIKU  YA MFUKO WA AFYA YA JAMII MIJINI WA TIBA KWA KADI (TIKA) KOROGWE MJI AMBAPO LENGO LA MKUTANO HUO NI KUCHUKUA MAONI NA KUWAELEZA JINSI TIKA INAVYOFANYA KAZI

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE ,MRISHO GAMBO AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA WADAU SIKU YA MFUKO WA AFYA YA JAMII MIJINI WA TIBA KWA KADI(TIKA)

MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA LA AFYA(NHIF)MKOA WA TANGA,ALLY MWAKABABU AKIELEZEA  UMUHIMU WA  MATUMIZI YA TIBA KWA KADI (TIKA)MBELE YA MGENI RASMI AMBAYE NI MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KOROGWE MJI, NA DIWANI WA KATA YA KILOLE ,ANGELO BENDERA AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIZUNGUMZA KWENYE MKUTANO HUO

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KOROGWE MJI,LEWIS KALINJUNA AKISISITIZA UMUHIMU WA JAMII KUJIUNGA NA MFUKO HUO KATIKA MKUTANO HUO

AFISA MATEKELEZO NA URATIBU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)-SINGIDA ISSAYA SHEKIFU AKITOA UZOEFU WAKE KILA MMOJA WILAYA YA IRAMBA -SINGIDA JINSI WANANCHI WALIVYOFADIKA KUPITIA TIKA.

VIONGOZI WA DINI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI MJI WA KOROGWE WAKIFUATILIA KWA UMAKINI MIJADALA ILIYOKUWA IKIENDESHWA






MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU,CHIKU GALLAWA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA MFUKO TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF  MARA BAADA YA KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU

0 comments

WAUGUZI NA MADAKTARI WASITISHA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA NI BAADA YA HOSPITALI KUKUMBWA NA MAFURIKO

WAUGUZI NA MADAKTARI WASITISHA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA NI BAADA YA HOSPITALI KUKUMBWA NA MAFURIKO


 Huu ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita kati kati ya Hospitali ya Palestina amapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya Hospitali hiyo
 Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha
 Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali
 Kushoto ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali katika makazi ya watu.
 Hii ndio hali halisi ya Chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya  Sinza Palestina
 Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya Hospital hiyo
 Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate hudumiwa
 Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
 Hapa hata hapapitiki
 Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
 Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha
 
 Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
 Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
 Huu ndio Mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya Mtaro huo kuziba.Picha zote Zimeletwa hapa http://kilinyepesi.blogspot.com/ na Dar es salaam yetu
--
Mapema mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es salaam kumesababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara , nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.
 
Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014  zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa maji hayo. Na wengine kukimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
 
Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tuu lakini yalikuwa ni Machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.
 
Baada ya mvua hiyo kwisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Akiongea kwa Simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa. 
 
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
 
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema  wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.
0 comments

CHAUSTA WASHINDWA KUFANYA KAMPENI KALENGA

CHAUSTA WASHINDWA KUFANYA KAMPENI KALENGA



IKIWA zimebaki takribani siku kumi ili kufungwa kampeni za kugombea ubunge katika jimbo la Kalenga, mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Haki na Ustawi (CHAUSTA), Richard Minja anatarajia kuzindua kampeni kesho katika kijiji cha Wasa Kata ya Maboga.
Akizungumza na mtandao huu leo kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa CHAUSTA, Mwaka Mgimwa amesema licha ya kuchelewa kuanza kampeni watafanya kazi kubwa ili kuhakikisha wanapata ushindi katika jimbo hilo.
Mgimwa amesema anatoka kwenye vikao vya Bunge maalum la Katiba linalofanyika mjini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni hizo ambapo baada ya uzinduzi watahakikisha wanatafanya kata kwa kata na kijiji kwa kijiji katika muda huo uliobaki.
Tangu kuanza kwa kampeni Februari 19 mwaka huu, Chama hicho kimekuwa kikishindwa kufanya kampeni kwa sababu zilizoelezwa kuwa Mgombea huyo yupo nje ya mji kwa shughuli za kijamii na kushindwa kufuata ratiba kama ilivyo.
Hata hivyo katika ratiba chama hicho kinaonekana kutokuwa na muda mwingi wa kampeni  kulinganisha na vyama vya CCM na Chadema vinavyoonekana kuwa na muda mwingi wa kufanya kampeni.
Kampeni za jimbo la Kalenga kwa  chama cha CHAUSTA  zilitarajiwa kuzinduliwa rasmi tangu February 22 katika kijiji cha kibaoni kata ya Ifunda jimboni humo ambapo tangu ratiba kuanza chama hicho hakijawahi kuonekana kufanya mkutano hata mmoja.
Mtandao huu ulipomtafuta mgombea huyo kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi zaidi juu ya kukwama kwa kampeni katika chama chake amesema hangeweza kuzungumza chochete kwa kuwa yupo nje ya mji.
“Nipeni muda kwa sasa siwezi kuliongelea hilo suala nitawapeni jibu kesho asubuhi. Kampeni zipo nyingi mimi ninafanya  za kimya kimya sio lazima nifanye kampeni na matarumbeta, magari na mziki ndio mjue nafanya kampeni kwasababu kila mtu anatumia staili yake ya kufanya kampeni” amesema Minja.
Hata hivyo alipododoswa zaidi amesema kuwa kutumia hela nyingi kwenye kampeni ni kuwadanganya wananchi kwasababu wao ndio wanashida nyingi na wanahitaji msaada kutoka kwa viongozi hivyo ni bora pesa zitunzwe ili baada ya ushindi zitumike kuwaletea maendeleo wananchi.
Hata hivyo mgombea huyo ametuma ujumbe mfupi kuwa bado yuko nje ya mji na anatarajia kurudi leo kwa ajili ya kuandaa shughuli za uzinduzi wa kesho katika kijiji cha Wasa Kata ya Maboga.
0 comments

KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata ili washinde katika mechi yao dhidi ya Prisons, mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Sokoine jiji mbeya.

KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata ili washinde katika mechi yao dhidi ya Prisons, mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Sokoine jiji mbeya.




Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
 
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata ili washinde katika mechi yao dhidi ya Prisons, mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Sokoine jiji mbeya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Logarusic alisema timu yote inahitaji ushindi katika mechi yao hiyo, hivyo jambo kubwa ni kuona vijana wake wanakuwa makini zaidi uwanjani.

“Tumepoteza pointi muhimu katika mechi iliyopita kwasababu ya wachezaji kutotumia ipasavyo nafasi za wazi wanazozipata, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limetugharimu.

“Naamini wakati huu wachezaji wote wanafahamu jambo gani muhimu wanapaswa kufanya uwanjani kwa ajili ya kuwapatia maatokeo mazuri, maana mpira ni mchezo wa makosa,” alisema.

Alisema kuwa kila mchezaji anaweza kufunga anapokuwa katika nafasi mzuri ya kufunga na kuhakikisha nafasi tatu za wazi wanazozipata moja wapo wanaibuka na ushindi.

Simba itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu za kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya JKT Ruvu, uliochezwa Jumapili iliyopita katika uwanja wa Taifa, mechi iliyowasononesha mashabiki wao.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger