SERIKALI YATAKIWA KUONDOA KWENYE VIFAA VYA UJENZI WA NYUMBA.
Na Elizabeth Kilindi,Mkinga.
MWENYEKITI wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasiri na Mazingira James Lambeli, ameitaka
serikali kuondoa kodi kwenye vifaa vya mradi wa ujenzi wa nyumba za
gharama nafuu unaoendeshwa na Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) ili
kumuwezesha mwananchi wa hali ya chini kuondokana na makazi duni.
Lembeli aliyasema hayo baada ya taarifa ya mradi huo iliyosomwa hapo juzi, mbele ya kamati hiyo na Kaimu Mkurugenzi wa uendeshaji wa shirika hilo, Benedict Kilimba na kueleza kuwa kodi za serikali zimesababisha bei ya nyumba hizo kuwa kubwa.
Lembeli aliyasema hayo baada ya taarifa ya mradi huo iliyosomwa hapo juzi, mbele ya kamati hiyo na Kaimu Mkurugenzi wa uendeshaji wa shirika hilo, Benedict Kilimba na kueleza kuwa kodi za serikali zimesababisha bei ya nyumba hizo kuwa kubwa.
Kwamujibu wa taarifa hiyo ni kwamba mfumo wa kuwataka wanunue vifaa vya ujenzi kwenye maduka maalumu kumeongeza gharama ya ujenzi huo na kufikia tsh mil, 31.3 kwa nyumba yenye vyumba viwili na tsh mil, 35.3 hadi tsh mil, 36.2 kwa vyumba vitatu bila VAT.
Aidha Kilimba alisema kuwa mbali na changamoto hizo shirika pia linalazimika kuilipa serikali kiasi cha tsh mil, 7 mpaka tsh mil, 10 kama kodi ya ongezeko la thamani VAT kutokana na manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa kila nyumba jambo lililosababisha nyumba hizo kuuzwa tsh mili, 40. 7 kwa nyumba ya vyumba viwili na tsh million 46. 3 hadi tsh mil, 48.2 kwa vyumba vitatu.
Hata hivyo alieleza kuwa kama shirika litaruhusiwa kutafuta maduka yenye unafuu na serikali ikaondoa kodi ya VAT mauzo ya nyumba hizo yangeweza kufikia tsh mili, 28 bei ambayo mtu wa hali ya chini angeweza kuimudu tofauti na ilivyo sasa.
Akizungumza baada ya taarifa hiyo, Lembeli alisema ni wajibu sasa kwa serikali kuonyesha moyo wa dhati katika kuwawezesha wananchi kumudu kubadilisha maisha yao ikiwemo hili la makazi bora ambayo ni haki ya kila mtu.
Aliahidi kubeba jukumu la kuishauri serikali kuondoa kodi ya VAT kwenye vifaa vya ujenzi wa nyumba zinazojengwa na mradi wa shirika hilo hasa zile zilizolengwa kwa ajili ya makazi bora kwa watu wa hali ya chini.
“Jamani sisi wanakamati yetu tumetembea katika nchi mbalimbali kama vile nchi ya Singopore, tumejionea na kujifunza jinsi serikali ya nchi hiyo inavyowawezesha watu wake katika makazi bora……..takriban asilimia 90 ya nyumba zilizojengwa na serikali ya nchi hiyo zimeuzwa kwa wananchi kwa bei nafuu, vipi sisi huku!” alihoji Lembeli.
Hata hivyo alidai kuwa taarifa ya shirika hilo kuhusu mazingira ya ujenzi wa nyumba hizo inaonyesha kwamba mtu wa kawaida hatakuwa na uwezo wa kuzinunua kutokana na ukubwa wa bei jambo alilolieleza kuwa linaondoa maana halisi ya azma iliyokusudiwa na serikali yenyewe ama wananchi walalahoi.
Post a Comment