NYOSSO ASEMA YANGA WALITOKA KIBAHATI MKWAKWANI
Beki wa
Coastal Union, Juma Said Nyosso amesema Yanga walikuwa na bahati zaidi katika
mechi yao jana.
Nyosso
amesema walikuwa na nafasi kubwa ya kuifunga Yanga kwa kuwa waliizidi sana.
Lakini
akasisitiza katika suala la mpira, ni vigumu kwa kulazimisha kitu ambacho
hakiwezekani.
“Tulijitahidi
kadiri ya uwezo wetu, tulikuwa katika nafasi nzuri ya kuifunga Yanga ingawa
naweza kusema mambo yalikataa tu.
“Sisi ndiyo tulicheza vizuri zaidi siku hiyo, lakini bahati haikuwa yetu,” alisema beki huyo wa zamani wa Simba.
Post a Comment