LOGARUSIC ATAKA WANAJESHI WASIOKATA TAMAA
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema
anataka kuwa na wachezaji wenye moyo wa ushindani na wasiokubali kushindwa.
Logarusic
amesema anaamini kuwa na washindani katika kikosi chake ni jambo la msingi
zaidi, na haamini watu wanaokata tamaa mapema.
“Kama
unakata tamaa mapema, basi hauwezi kufanya kazi na mimi. Nataka wapambanaji.
“Katika
maisha kuna mawimbi, hauwezi kusafiri baharini bila ya kukutana na mawimbi. Ukikata
tamaa mapema, hautafika unapokwenda.”
Logarusic
anaamini kuwa mmoja wa makocha wakorofi lakini amekuwa akisifika kwa kusimamia
suala la nidhamu.
Tokea
ametua Simba, inaonekana suala la nidhamu limeimarika zaidi na watukutu
wamekuwa na hofu.
Post a Comment