MKWAKWANI KUKARABATIWA TENA BAADA YA KUMALIZIKA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU
Na Oscar Assenga, Tanga.
UONGOZI wa Uwanja wa Mkwakwani umesema awamu ya pili ya ukarabati wa uwanja huo unatarajiwa kufanyika mara baada ya kumalizika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara mwaka huu lengo lao likiwa ufikie kwenye viwango vya kitaifa na kimataifa.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga, Gustav Mubba wakati akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo ambapo alisema suala la ukarabati wa uwanja huo ni mkakati wao waliojiwekea kila mwaka.

Mubba alisema mara baada ya uwanja huo kumalizika mashabiki wa soka mkoani hapa wanapaswa kuwa na nidhamu kwa kuacha kuingia uwanjani wakati mchezo ukiwa umalizika kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha uharibifu wa vitu vilivyopo uwanjani hapo. “Napenda kuwaomba mashabiki wa soka baada ya kumalizika mpira wawe na nidhamu waache kuingia uwanjani baada ya kumalizika mechi kwani baadhi yao wanachana nyavu za magoli kitendo ambacho kinaleta usumbufu mkubwa sana “Alisema Mubba.
Aliwataka mashabiki wa soka wajifunze nidhamu ya matumizi ya uwanja hasa kwenye mechi ya Yanga na Coastal Union wa wale wanaotokea Dar es Salaam na mikoa mengine kuja kushuhudia mechi hizo wawe wastaharabu na kuacha kuleta vurugu.
Post a Comment