Featured Post Today
print this page
Latest Post

RAS CHIMA AWAFUNDA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO,AWATAKA MADEREVA KUACHA KUPAKIA MISHIKAKI

RAS CHIMA AWAFUNDA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO,AWATAKA MADEREVA KUACHA KUPAKIA MISHIKAKI

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA,SALUM CHIMA AKISALIMIANA NA VIONGOZI WA MBALIMBALI  MKOANI HAPA KUSHOTO NI KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA,JUMA NDAKI


KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA,SALUM CHIMA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA MKOA WA TANGA WAKATI WA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA AMBAPO KIMKOA ILIADHIMISHWA KWENYE VIWANJA VYA TANGAMANO LEO

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA,JUMA NDAKI AKIONGEA

MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI,MKOA WA TANGA,ABDI ISANGO AKIFUATILIA VIKUNDI VYA SANAA VILIVYOKUWA VIKITUMBUIZA KWENYE KILELE HICHO LEO








0 comments

MIGOGORO YA ARDHI,MIPAKA NI TISHIO WILAYAINI HANDENI.

MIGOGORO YA ARDHI,MIPAKA NI TISHIO WILAYAINI HANDENI.

NA MWANDISHI WETU, HANDENI
SERIKALI Kuu kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Handeni na Mkoa mzima wa Tanga, wameombwa kuingilia kati mgogoro mzito wa ardhi katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, ili kuepusha hatari inayoweza kutokea, ikiwamo vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Hayo yamesemwa juzi na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Handeni Kwetu Foundation inayofanya ziara katika maeneo mbalimbali, hususan ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, baada ya kuzinduliwa Mei 8 mwaka huu.

Wakizungumza kwa uchungu mkubwa, wananchi hao walisema kuwa hali ni mbaya, maana kijiji chao kimeendelea kutekwa na kubaki eneo dogo lililoanza kuibua chuki za wazi kwa wananchi.

Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Alhaj Ally Yasin Ling’ande, alisema kiuhalisia hakuna kijiji cha Komsala, kwakuwa hawana eneo la ardhi, hasa baada ya wilaya Korogwe kuingia kwenye eneo lao kwa kufikia hata kujenga mnada wa ng’ombe.

“Ukiaangalia usawa palipojengwa mnada, utaamini kuwa hata kwenye shule ya Msingi Komsala pia patakuwa ni eneo la Korogwe, ingawa si sahihi kulinganaa na ramani ya mwaka 1978, jambo linaloonyesha kuwa huu ni mzozo utakaoweza kumwaga damu,” alisema.

Naye William Seif alisema mbali na mipaka hiyo kuwa tata, pia kumekuwa na idadi kubwa ya wageni kumiliki heka zaidi ya 130 na bado wanaingia kwa wenye heka tatu wakiamini kuwa uwezo wao kifedha unawafanya wamudu kesi zinazoendeshwa kwenye mabaraza ya Kata na wao kupata haki.

“Masikini akionewa anakimbilia kwenye Bazara la Kata, lakini huko kumekuwa na danadana nyingi, ukizingatia kuwa siku zote mkono mtupu haulambwi, ndio maana tunaoimba serikali ya wilaya ya Handeni, mkoa na wadau wengine wa ardhi kuja kujionea bomu hili linalosubiriwa kuripuka hapa kwetu,” alisema.

Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bashiri Wabu, alisema kuwa ardhi katika kijiji chao imeuzwa kiholela kwa watu wenye nazo bila kufuata sheria za ardhi, ikiwamo ya kuandaa mkutano wa wananchi wote.

“Kuna watu hawana maeneo kabisa ya kulima, wakati watu wachache wanamiliki maeneo makubwa ambayo hata kuyalima yote hawana uwezo huo, jambo linalokera na kuudhi mno kila tunapoliangalia suala hili katika kijiji chetu,” alisema Wabu, akiungwa mkono pia na Hemed Ngona, Kombo Twaha, wakisisitiza kuwa sheria za ardhi na utawala bora hazifuatwi katika kijiji chao.

Katika mkutano huo ulioanza saa 9 alasiri na kumalizika saa 12 jioni, ulihudhuriwa na watu wengi, huku idadi kubwa ikiegemea katika kero ya ardhi na mipaka.

Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Komsala anayemaliza muda wake, Mwanaidi Said, alisema kero kubwa katika kijiji hicho ni mipaka iliyoshindwa kutatuliwa na viongozi wa juu, licha ya kupeleka malalamiko yao mara kadhaa.

“Kijiji cha Komsala sasa ni kama kitongoji tu, maana kimechotwa katika pembe zote na ndio maana hata wenzetu wa Korogwe wamekuja kujenga mnada wa ng’ombe kwa madai kuwa ni kwao, jambo ambalo hata mwenyekiti atakayefuata litamuumiza kichwa,” alisema na kuwafanya wananchi wapatwe na hofu.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo aliyetumia muda huo kuaga wananchi wake, sekeseke la mipaka limeshindwa kutatuliwa, huku akiwataka viongozi kulipa kipaumbele kabla ya matatizo hayajakikumba kijiji chao pale wananchi hao watakapotafuta haki yao.

Naye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, aliwashukuru viongozi wa serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kuwapa ushirikiano, ikiwamo kuruhusu kutembelea katika vijiji mbalimbali kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha utawala bora.

“Naomba niwatoe hofu Watanzania wote kuwa mikutano hii ya hadhara hairatibiwi na chama chochote cha siasa, hivyo tunaomba tushirikiane kwa ajili ya kufanikisha maendeleo, hasa kama wananchi watahudhuria mikutano wanapoitwa na viongozi wao,” alisema.

Ziara ya Handeni Kwetu Foundation ilianzia Kata ya Misima, ambapo wananchi wengi wameiunga mkono taasisi hiyo yenye lengo la kuwakomboa wananchi kwa kutoa elimu na kuhamasisha maendeleo ya jamii.
0 comments

ASKOFU KILAINI, NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA

ASKOFU KILAINI, NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini.

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.(P.T)
Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni).
Akizungumza kwa simu jana, Askofu Kilaini alisema Rugemalira hupendelea kuchangia kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye peke yake aliyempatia mchango, bali kuna watu wengine wengi ambao wameshampatia na kazi yake ni kuipokea na kuifikisha sehemu husika.
Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake, simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena.
Hata hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na Gazeti la Mawio toleo la jana akisema fedha alizozipokea kutoka kwa Rugemalira ni kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kanisa Katoliki.
"Ndiyo nimepokea fedha kutoka kwa James na hii siyo mara ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya kijamii," alisema Askofu Kilaini.
Alipotakiwa na gazeti hilo kuwataja wengine waliochangia kanisa lake na kama nao wamechanga kutoka kwenye fedha za akaunti ya escrow, alisema yeye hayumo kwenye michango hiyo.
Alipoulizwa anawezaje kusema hayumo kwenye orodha ya waliopewa fedha kutoka akaunti ya escrow wakati anakiri kuwa aliingiziwa mamilioni ya shilingi na Rugemalira, alisema michango inayoletwa kwake haina siri, hivyo wezi halisi ndiyo wakamatwe.
"Michango inayoletwa kwangu haina siri, shikeni wezi halisi," alisema.
Askofu Nzigirwa
Kwa upande wake, Askofu Nzigirwa ambaye alirithi kiti cha Kilaini, cha Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam ameeleza kushtushwa kwake na ripoti ya PAC iliyomtaja yeye na Kilaini kuhusika katika uchotwaji wa Sh306 bilioni za escrow.
Hata hivyo, kiongozi huyo alisema anaandaa taarifa itakayofafanua kwa kina namna ambavyo fedha hizo zinazodaiwa zilitoka katika akaunti ya escrow zilivyoingizwa katika akaunti yake pamoja na hoja na maswali mengi yanayoulizwa na wananchi hasa waumini wa Katoliki kuhusiana na tuhuma hizo.
"Hizo taarifa zimenishtua sana. Bado nashangaa inakuwaje mimi naambiwa nimechota fedha kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow," alisema Nzigirwa alipokuwa akizungumza na gazeti hili jana.
Nzigirwa alisema anachofahamu hadi sasa fedha zilizoingizwa katika akaunti yake hazihusiki na escrow lakini atafanya uchunguzi ili kupata undani wa fedha hizo na majibu yote yatakuwa katika taarifa atakayoitoa kwa vyombo vya habari siku yoyote kuanzia leo.
(CREDIT: MWANANCHI)
0 comments

A BETTER WORLD YASAIDIA UJENZI VYOO BORA MOMBO

A BETTER WORLD YASAIDIA UJENZI VYOO BORA MOMBO 

 

 

 

TAASISI ya A BETTER WORLD ya Canada imesaidia ujenzi wa matundu ya vyoo 16 yaliyogharimu Mil. 16.5 kwa shule ya msingi Misajini iliyopo Mombo wilayani Korogwe.


Taarifa hiyo imetolewa na Mwalimu wa Shule hiyo Elizabeth Mathew kwa Muasisi wa Shirika hilo nchini Eric Rajahamba kwenye uzinduzi wa mradi huo unaolenga kuboresha afya za wanafunzi.

Mwalimu Mathew amesema amesema kufadhiliwa kwa mradi huo ni matokeo mazuri ya mahusiano Mtanzania Azidi Kaoneka na taasisi hiyo ambae pia aliwai kuwaunganisha na wafadhili waliofanikisha mradi wa maji na upanuz wa madarasa.

 

1 comments

World Vision Waacha Wosia Ulinzi Kwa Watoto.

World Vision Waacha Wosia Ulinzi Kwa Watoto.

 
Shirika lisilo la Kiserikali la World vision Tanzania cluster ya Korogwe limeiomba jamii kuendeleza juhudi za shirika hilo walizozifanya kwa miaka kumi na tano katika tarafa ya Magoma wilayani Korogwe za kumlinda mtoto kwa kuhakikisha anapata huduma na haki zake zote za msingi.
Ombi hilo limetolewa jana na  mratibu wa mradi uliokuwa ukishughulikia maendeleo ya Magoma( Magoma ADP)  George Banyenza katika hafla ya kutia saini hati za makabidhiano iliyohudhuriwa na Watendaji wa World vision, watendaji wa halmashauri ya wilaya Korogwe,Diwani wa kata ya Magoma,Maafisa tarafa na Mtendaji wa kata hiyo, wenyeviti wa vijiji vya kata hiyo na wanufaika wa mradi huo iliyolenga  kukabidhi  rasmi majengo ya ofisi yaliyokuwa yakitumiwa na mradi huo kwa Serikali .
Banyenza alieleza kuwa kwa muda wa miaka kumi na tano World Vision kwa ufadhili wa watu wa ujerumani imekuwa ikiisaidia jamii ya tarafa ya Magoma kupitia watoto kupata huduma za elimu,afya na maji sambamba na kupinga ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha wanapata huduma zote za msingi.
“ADP Magoma imefikia tamati sasa lakini kwa kipindi chote tumekuwa tukiisaidia jamii  kupitia watoto hivyo tunaomba jengo na rasilimali zake tunazoacha ziwe chachu kwa jamii  kuendeleza ulinzi na usalama wa mtoto wa Magoma.” Alieleza Banyenza.
Katika hatua nyingine Meneja miradi Mwandamizi wa World vision  kanda ndogo ya Korogwe Sylvester Masanja, alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kuwa mlezi wa asasi ya jamii ya UKIMAMA iliyokuwa ikilelewa na mradi huo sambamba na kuwapatia chumba kimoja katika jengo hilo kwa ajili ya shughuli za asasi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Lucas Mweri aliyepokea hati za makabidhiano ya jengo na rasilimali zake aliahidi kutunza rasilimali hizo na kuhakikisha zinatumika kwa matumizi yenye tija kwa jamii.
 Magoma ADP imeikabidhi Serikali jengo lenye thamani ya Tsh 68,480,000/- walilolijenga mwaka 2010 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kusaidia watoto na jamii tarafa ya Magoma ambayo imefikia mwisho wa utekelezwaji wake. Stori & picha na Fatna Mfalingundi-Afisa habari Halmashauri ya Wilaya Korogwe
0 comments

NIPO MKOANI MOROGORO MCHANA HUU WA LEO, JUMAMOSI NOVEMBA 15.

NIPO MKOANI MOROGORO MCHANA HUU WA LEO, JUMAMOSI NOVEMBA 15.


    HAPA NI ENEO LA MASIKA MKOANI MOROGORO, KAMA LINAVYOONEKANA    MCHANA HUU, KWA MBALI INAONEKANA MILIMA YA ULUGULU



   MORO YAPENDEZA NI WIMBO WA MAREHEMU MBARAKA MWISHEHE, HAPA NI MSIKA
0 comments

WANAODAIWA KUWA NI WAVUVI HARAMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO BAADA YA KULIPUKIWA NA MABOMU YAO WAKATI WAKIVUA

WANAODAIWA KUWA NI WAVUVI HARAMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO BAADA YA KULIPUKIWA NA MABOMU YAO WAKATI WAKIVUA

Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. (Picha na Elizabeth Kilindi)
 Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono.
 Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na barutiwakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono.
  Mmoja wa majeruhi waliolipukiwa na baruti wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. 

Elizabeth Kilindi, Tanga
Wakazi wawili wa kata ya Tangasisi tarafa ya Pongwe wilayani Tanga wamejeruhiwa vibaya viungo mbalimbali vya mwili  kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivua kwa kutumia dhana za uvuvi haramu kwenye kisiwa cha Karange.

Tukio hilo limetokea mnamo Novemba 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kisiwa  ambapo majeruhi hao wakiwa kwenye ngalawa yenye namab za usajili TTA 315 wakati wakijianda kutegesha baruti hizo ndipo zilipowalipukia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Freisse Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majeruhi hao kuwa ni Hamis Omari ambaye amekatika mkono wa kulia na ameumia jicho la kulia, huku majeruhi mwingine Adamu Selemani amekatika mikoni yote miwili, pamoja na kupoteza macho yote mawili.

“Hali ya majeruhi wote wawili ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo ni mbaya hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uvuvi haramu ulivyo na madhara makubwa kwa jamii pamoja na viumbe wa baharini “alisema Kamanda Kashai.

Kamanda Kashai alitumia fursa hiyo kuwa taka wakazi
wanaoishi maeneo ya bahari kutoa taarifa ya watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ili kuweza kuwachukulia hatua mapema kabla ya kutokea kwa madhara zaidi.
0 comments

Upekee wa Hifadhi ya Saadani usiotangazwa

Upekee wa Hifadhi ya Saadani usiotangazwa


Kila hifadhi ya taifa ina upekee wake. Na hicho hukifanya kuwa kivutio kwa watalii. Hifadhi ya Taifa ya Saadani ina vivutio vya kihistoria kama vile wanyama, mito na bahari. Nadhani ni hifadhi pekee inayoweka pamoja vivutio vyote.
Kihistoria Hifadhi ya Saadani inapakana au kuhifadhi miji ya kihistoria kama Saadani wenywe, Utondwe, Kipumbwi na Mkwaja, Pangani, Buyuni Ukuu na Buyuni Kitopeni ambayo ingawa sasa haijulikani tena.
Katika zama zake ilikaribisha wageni wa kimataifa, au kuwa miji ya kibiashara (ya maliasili na watumwa) na kuwakaribisha wakoloni na kujenga miji.
Saadani ulikuwa mji mkubwa sana wakati wa ukoloni


 wa Wajerumani na pia kaburi la yule mmishenari maarufu aliyekuja kueneza Ukristo, hasa Mombasa, Tanga na Kilindi, Johannes Rebmann liko hapo hadi leo.
Hadi leo Kipumbwi bado ni bandari muhimu ya majahazi inayounganisha Wazanzibari na Watanganyika kwa kufanya safari kati ya kijiji hicho cha pwani na bandari kuu ya awali – Mkokotoni. Safari hizo ziko kila siku.
Miji ya Pangani, Bagamoyo na kijiji kilichopotea cha Utondwe vina mpatia fursa mtalii kuvifikia wakati anapotembelea hifadhi hiyo.
Utondwe unaandikwa na Wareno kama mji wa mashamba ya chumvi na askari wa Kizaramo wapiga mishale wazuri. Ushahidi ni msikiti wa kale uliopo hadi sasa huko Kitame, ingawa hautumiki.
Saadani ni hifadhi inayopakana na mito mitatu. Ruvu uko mbali lakini kuna Pangani na Wami. Mito hii mitatu kwa pamoja hukutana huko baharini na kutengeneza mkondo hatari wa Nungwi unaoleta vurugu katika majira fulani fulani.
Serikali ya Zanzibar kama ingekuwa na uwezo wa kifedha ungeweza kutengeneza bomba la kuvuta maji baridi kutoka kwenye kine kirefu cha Nungwi, yanayotokana na Ruvu, Wami na Pangani, mito mitatu inayopangana na hifadhi ya Saadani.
Pia, ndani ya mito hiyo unajifunza maisha na uhifadhi unaofanyika wa maisha ya majini na baharini ya wanyama na mimea.
Wakati ukiwa Mto Wami unajifunza maisha ya baharini na wanyama wake, Mto Pangani una hifadhi kubwa ya mapito ya kihistoria na biashara- utumwa, katani, mali ya asili, hasa meno ya tembo na nazi mbichi na mbata.
Ukisafiri katika Mto Pangani hadi huko ndani nchi kavu unakutana na vituo vya kihistoria ikiwamo mahali Bushiri bin Salim alipoishi, Matakani na Kijiji cha Bushiri.
- Mwananchi
0 comments

SPIKA MAKINDA APONGEZWA, PINDA AFUNGA MKUTANI WA KUHIFADHI WANYAMAPORI

SPIKA MAKINDA APONGEZWA, PINDA AFUNGA MKUTANI WA KUHIFADHI WANYAMAPORI

unnamed
unnamed2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwenye viwanja  vya  Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2014 katika tafrija  ya kumpongeza Spika kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Mabunge ya  SADEC . Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah na wapil kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela  Kairuki na kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dr. Pindi Chana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed3Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda  (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa katiba na Sheria, Angela Kairuki  (katikati) alipotoa maelezo kuhusu zawadi ya picha  ambayo wabunge walimzawadia Spika Makinda katika tafrija ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa spika wa Mabunge ya SADEC iliyofanyia kwenye viwanja vya Bunge mjioni Dodoma Novemba 7, 2014.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed4Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda  (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa katiba na Sheria, Angela Kairuki  (katikati) alipotoa maelezo kuhusu zawadi ya picha  ambayo wabunge walimzawadia Spika Makinda katika tafrija ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa spika wa Mabunge ya SADEC iliyofanyia kwenye viwanja vya Bunge mjioni Dodoma Novemba 7, 2014.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed5Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  ambako alifunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori  na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori uliofanyika mjini Arusha Novemba 8, 2014.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed6 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza  na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wapili  kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri (kulia) baada ya kufunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori  na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli.Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Dkt Richard Sezibara(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed7 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza  na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wapili  kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri (kulia) baada ya kufunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori  na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli.Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Dkt Richard Sezibara(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments

Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema

Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akizungumza na  Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya
Johns Hopkins na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi(kulia) baada
ya kuwasili katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore,
Maryland,  Marekani kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo
uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.(Picha na Fred Maro) unnamed2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa
Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha
upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo
Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua
muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
…………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa
Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini
ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete
kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014
0 comments

JANUARY MAKAMBA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO BUMBULI VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 20,AWEKA MKAKATI WA KUPATA TIMU YA LIGI KUU SIKU ZIJAZO

JANUARY MAKAMBA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO BUMBULI VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 20,AWEKA MKAKATI WA KUPATA TIMU YA LIGI KUU SIKU ZIJAZO

KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI WILAYANI LUSHOTO,HOZA MANDIA AKIWAKABIDHI VIJANA JEZI WA MICHEZO LEO

KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI WILAYANI LUSHOTO,HOZA MANDIA AKIWAKABIDHI VIJANA JEZI WA MICHEZO LEO

HAPA KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI HOZA MANDIA AKIWAKABIDHI VIJANA HAO FEDHA TASLIMU

KUSHOTO NI KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI HOZA MANDIA AKIMKABIDHI MPIRA DIWANI WA KATA YA USAMBARA
MASHABIKI WA SOKA TAMOTA WAKIWA WAMESHIKILIA VITITA VYAO LEO

MASHABIKI WA MAHEZANGULU WAKIFUHAIA BAADA YA KUKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO

KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI HOZA MANDIA KUSHOTO AKIWAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO TIMU YA TAMOTA




KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI HOZA MANDIA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MASHABIKI WA SOKA WA  MILINGANO

MASHABIKI WA KATA YA VUGA WAKIWA NA FURAHA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA JEZI NA VITITA VYAO

KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI HOZA MANDIA KUSHOTO AKIMKABIDI VIFAA VYA MICHEZO KIONGOZI WA TIMU YA MILINGANO

0 comments

KINANA AHITIMISHA ZIARA TANGA

KINANA AHITIMISHA ZIARA TANGA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwapungia mkono wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Tangamano, jijini Tanga jioni ya leo, alipokuwa akihitimisha ziara ya siku 11 katika Mkoa wa Tanga.
Kinana akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa hadhara, jijini Tanga leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akipanda ngazi kwenda jukwaani wakati wa mkutano huo.
 Bajaji zikiongoza msafara wa Kinana kwenda kwenye mkutano wa hadhara.
 Msafara wa pikipiki ukiongoza msafara wa Kinana jijini Tanga.


 Bodaboda zikiongoza msafara wa Kinana
Kinana akipiga Saluti ikiwa ni ishara ya kuwasalimia wananchi katika mkutano huo
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara jijini Tanga
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya 2010
wa Jimbo la Tanga Mjini, Omari Nundu akielezea jinsi miradi ilivyotekelezwa  katika jimbo hilo
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wapinzani walioamua kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara
Kinana akivalishwa kanzu aliyopewa na wazee wa Tanga baada ya kufurahishwa na hotuba yake
Wazee wa Tanga wakimpatia zawadi ya kiti maalumu Kinana
Wananchi wakiwa na hamu ya kupeana mkono na Kinana baada ya mkutano kumalizika
Kinana akiwa katika vazi alilopewa zawadi na wazee wa Tanga baada ya kufurahishwa na hotuba yake
Kinana akiondoka baada ya kumaliza mkutano
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger