MALAIKA MUSIC BAND KUWASHA MOTO TANGA NOVEMBA 23.
Na Oscar Assenga,Tanga.
BENDI Mpya ya Malaika Music
Bendi inatarajiwa kufanya uzinduzi wa aina yake mkoani Tanga Novemba 23 mwaka
huu katika ukumbi wa Tanga Hotel jijini Tanga ikiwa na waimbaji wake wote.
Akizungumza na blog hii,Meneja
Masoko wa Bendi hiyo,Juma Abajalo alisema maandalizi ya onyesho hilo
yanaendelea vizuri ambapo kabla ya kuja mkoani hapa itafanya uzinduzi wake
Novemba 15 mwaka huu Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salaam na baada ya
hapo wataelekea mkoani Morogoro na hatiamye kutua mkoani Tanga.
Abajalo alisema lengo la
kuanzishwa bendi hiyo ni kuhakikisha wanakata kiu za wapenda mziki wa dansi
hapa nchini kutokana na kusheheni wasanii nguli ambao wanajua kulitawala
jukwaaa.
Meneja huyo alisema katika
onyesho hilo,Rais
wao Christiani Bella “Obama akisaidiwa na marapa pembeni Totoo Ze Bingwa,Fadii
na mpiga kibodi maarufu nchini Andrew Sekedia.
Aidha aliwataka wakazi wa
mkoa wa Tanga kukaa mkao wa kula ili kuweza kusikiliza masauti makali ya
Christiani Bela “Obama”na wasanii wengine ambao wanaunda bendi hiyo
watakaowasha moto siku hiyo.
“Ninachoweza kusema burudani itakayopatikana
hapo itakuwa sio ya mchezo hivyo nawaomba wakazi wa mkoa wa Tanga kuhakikisha
wanapata nafasi ya kushuhudia uzunduzi huo ambao utakuwa wa aina yake “Alisema Abajalo.
Post a Comment