Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akimtambulisha Mhe. Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Kenya kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa
pamoja na Waandishi hao kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya kwa hotuba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
aliyoitoa hivi karibuni kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Katika hotuba hiyo Mhe. Rais Kikwete alieleza msimamo wa
Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
|
Mhe. Amina Mohammed akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari huku Mhe. Membe akisikiliza. |
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John
haule (wa pili kulia) akimsikiliza Mhe. Mohammed (hayupo pichani)
alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya
kwa Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa
Idara ya Afrika, Balozi Vincent Kibwana (wa pili kushoto) na Mjumbe
kutoka Kenya. |
|
Post a Comment