Siasa Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza
Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati
akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Meatu mjini Meatu, ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja
Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa
ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba
kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya
hiyo, Akongeza kwamba jambo la pili ni kwamba Ndugu Abdulrahman Kinana
ni rafiki yake wa muda mrefu kwa hata wakati wakisoma shule wote
walisoma moshi Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John
Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati
alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia
shilingi Milioni moja "Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana
kwa hoja" amemaliza Shibuda.
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MEATU
SIMIYU)
Post a Comment