Ili kuchochea kasi ya maendeleo, watendaji wilayani Handeni waapa kufunga mkanda

Ili kuchochea kasi ya maendeleo, watendaji wilayani Handeni waapa kufunga mkanda

Na Kambi Mbwana, Handeni
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, amesema kwamba wameamua kufunga mkanda kuhakikisha kuwa kasi yao inazidi kushika kasi kwa kufanya kazi bila kuchoka na kuonyesha mfano kwa watendaji wengine wote.
Katibu Tawala wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog ofisini kwake, Ticky alisema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakifunga mkanda kuhamasisha pia ufanyaji wa kazi za kijamii badala ya kusubiria kutoa maagizo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani
Alisema hilo limechangia kuharakisha maendeleo katika wilaya yao, sambamba na kutoa mwanya wa kusubiri ‘madudu’ kutoka kwa watendaji wavivu.

“Sisi kwa pamoja na Mkuu wetu wa wilaya, Muhingo Rweyemamu, tumeamua kufanya kazi kwa nguvu zote, zikiwamo zile za kufyatua matofali, usafi na mengineyo yote.
“Mara kwa mara haya yamekuwa yakifanywa kwa kutoa maagizo tu, jambo linalochelewesha maendeleo, hivyo tunahakikisha kuwa kasi hii inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa maendeleo ya wote,” alisema.
Tangu kuteuliwa kushika nafasi ya DC wa Handeni, Muhingo amekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watendaji wote wa wilaya hiyo sanjari na wananchi kwa ujumla, jambo linaloweza kuchangia maendeleo ya haraka kwa wilaya hiyo ya Handeni.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger