MTOTO WA MIAKA 8 AOLEWA NA MWANAUME WA MIAKA 38.
Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samson (38), mkazi wa Kijiji cha Mindukeni, Tarafa ya Tarawanda katika Wilaya ya Bagamoyo,
Pwani amefanya maajabu ya milenia baada ya kudaiwa kuoa mtoto mwenye umri wa miaka nane .
Habari za kiuchunguzi zilisema kuwa mwanaume huyo ambaye tayari alishaoa mke wa kwanza, alidaiwa kumtorosha mtoto huyo nyumbani kwao, Iringa.
Ilidaiwa kuwa Samson alifanya tukio hilo kwa kushirikiana na mjomba wa mtoto huyo, wakati akichunga mbuzi mkoani Iringa.
Habari zilieleza kuwa baada ya Samson kumtorosha mtoto huyo kijijini kwao alimpeleka kijijini Mindukeni, Pwani na kumuweka kinyumba akiwa ni mke wake wa pili.
Ilidaiwa kwa kuwa mtoto huyo analingana na watoto wake kwa mke wa kwanza, alimweka chumba kimoja na wanaye.
Kabla ya ishu kubumburuka, Samson alikuwa akiishi na mtoto huyo akiwa ni mke mdogo huku akimtumia kufanya kazi mbalimbali kama kuchunga mbuzi, kuchota maji kisimani na kusaidia kubeba au kulea watoto wa mke mkubwa.
Kwa mujibu wa mtoto huyo, hadi sasa hajui alifikaje kijijini hapo na wala hatambui jinsi ya kurudi kwao kwani walimuiba tu.
Alisema baada ya kufikishwa kijijini hapo, alikuwa akilala chumba cha watoto na mwanaume huyo akitaka kumuingilia anaingia chumbani humo na kufanya naye mapenzi kisha kurudi kwa mke mkubwa.
“Nilikuwa naumia wakati akiniingilia, alikuwa anakuja chumba tunacholala na watoto wake wengine, ananichukua pembeni na kufanya mapenzi, akimaliza anarudi kwa mke mkubwa,” alisema mtoto huyo na kuongeza:
“Kusema kweli mwanzoni nilikuwa nasikia maumivu makali hadi nilipokuja kuona ni kitu cha kawaida.”
Mtoto huyo alisema kuwa kila kulipokucha alikuwa anaona aibu kwani wale watoto wengine wanalingana naye hivyo alikuwa akiumia kufanyiwa kitendo kama hicho cha ukatili na mtu ambaye ni sawa na baba yake.
Aliendelea kusema kuwa aliumia kupelekwa katika kijiji hicho na kuishi na mwanaume huyo na tayari ameshakaa miaka minne kama mke wake, akimuingilia mara kwa mara na kumsababishia maumivu.
“Nimeishi naye muda mrefu kama miaka minne, natamani kurudi kwetu nikasome,” alisema mtoto huyo.
Kwa upande wake mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live cha EATV, Joyce Kiria alifika katika kijiji hicho na baadaye alikwenda katika Kituo cha Polisi Bagamoyo kisha kuchukua askari usiku wa manane ambapo Samson alitiwa mbaroni na hadi sasa yupo mahabusu huku mtoto huyo akisubiri kuanza shule.
Habari
hii ni ya kusikitisha kwa sababu huu ni zaidi ya ukatili kwa watoto
wadogo, ili kujua na kuona mengi zaidi yaliyotokea kupitia runingani,
usikose kuangalia Kipindi cha Wanawake Live cha EATV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio la kuolewa kwa mtoto huyo, serikali ya Rais Jakaya Kikwete kupitia Jeshi la Polisi chini ya IGP Said Mwema wanatakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaofanya ukatili katika jamii hasa kwa watoto wasio na hatia.
Post a Comment