TANZANIA, CONGO NA BURUNDI WAUNDA MUUNGANO WAO BAADA YA KUTENGENGWA

TANZANIA, CONGO NA BURUNDI WAUNDA MUUNGANO WAO BAADA YA KUTENGENGWA

Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.
  
Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.

Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.
Mkutano wa ujirani mwema
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.
Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia.
Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC,” alisema Sitta.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.
Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo,” alisema Sitta.
Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni – Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.
Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger