RAIS WA MALAWI JOYCE BANDA ASHITAKIWE UMOJA WA NCHI ZA AFRICA

RAIS WA MALAWI JOYCE BANDA ASHITAKIWE UMOJA WA NCHI ZA AFRICA

Taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia mambo ya utawala bora na maendeleo nchini (The Center for Good Governance and Development in Tanzania -CEGODETA), imeitaka Serikali ya Tanzania kumshtaki Rais wa Malawi, Joyce Banda Umoja wa Nchi za Afrika (AU).

Taarifa ya taasisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya ilisema uamuzi huo ni kutokana na kauli za dharau za Banda dhidi ya viongozi wanaoshughulikia mgogoro wa Ziwa Nyasa.

“Serikali imshtaki kiongozi huyo wa Malawi AU ili aulizwe ana dhamira gani kwa Tanzania na Afrika kabla hajaleta madhara makubwa kwa nchi yetu na Bara zima la Afrika.

Waswahili husema ‘Mchelea mwana kulia hulia yeye’ na ‘Mdharau mwiba mguu huota tende’, maana yake ni kuwa inawezekana huyu mtu ana mtandao mbaya sana tusioujua, tufanye uchunguzi kuubaini,” inasema taarifa hiyo.

Inasema kuwa, mara tu baada ya kuingia madarakani Rais Banda alidai kuwa Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa asilimia 100 na Tanzania haina haki ya kulitumia ziwa hilo kwa njia yoyote ile.

Taarifa hiyo inasema kuwa, mgogoro huo kwa sasa uko kwenye jopo la usuluhishi la marais wastaafu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Rais Mstaafu, Joachim Chissano wa Msumbiji.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger