ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUOA BINTI WA MIAKA 18
Na Oscar Assenga,Tanga.
MZEE wa Miaka sabini
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuoa binti mwenye umri chini ya
miaka kumi na nane Mosa Hamisi kinyume cha sheria zilizopo hapa nchini.
Mkasa huo ulitokea Novemba 10
mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni ambapo mzee huyo tayari alishafunga
ndoa na binti huyo lengo likiwa ni kuishi naye kama
mke na mume.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tanga,Constatine Massawe alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza tayari jeshi linamshikilia
mtuhumiwa huyo pamoja na mama mzazi wa binti huyo.
Massawe alimtaja mzee huyo
kwa jina la Abdallah Tuppa (70)mkazi wa barabara kumi mbili na mama mzazi binti
huyo Batuli Tupa (35)ambaye anaishi barabara kumi na nne jijini Tanga.
Alisema tukio hilo liligunduliwa na wasamaria wema baada ya kuona binti
huyo anaozeshwa ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambapo
wakati polisi walipofika eneo hilo
walimkuta mzee huyo akidai mke wake ndipo walipomkamata.
Kamanda Massawe alisema askari
walifanikiwa kumuhoji binti huyo ambapo alisema umri wake ni zaidi ya miaka
kumi na saba hali ambayo ilipelekea kumuambia alete cheti chake cha kuzaliwa
ili kuthibiti umri huo.
Wakati huo huo,mtu mmoja
amekufa baada ya kugongwa na gari akiwa anaendesha baiskeli katika barabara ya
Segera –Chalinze.
Kamanda Massawe alisema tukio
hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 za usiku na
kumtaja dereva aliyesababisha ajali hiyo kuwa ni Abdallah Msangi (30) wa gari hilo aina ya fuso lenye
namba T390 DCB.
Massawe alimtaja aliyefariki
katika ajali hiyo kuwa ni Hamisi Saidi mkazi wa Michungwani ambapo alisema
chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva.
Post a Comment