DIWANI ATAKA SOKA LA DEEPSEA LIVUNJWE
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
DIWANI wa Viti Maalumu Kata
ya Chumbageni jijini Tanga kupitia chama
cha Mapinduzi (CCM)Saida Gadafi amelishauri baraza la madiwani kuridhia
soko la kuuzia samaki la deepsea livunjwe kuliko kila mwaka litengewe
sh.milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wake.
Gadafi alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa mipango miji jijini Tanga ambapo alisema fedha
hizo zinazotengwa hazionekani zinafanyia kazi gani kwa sababu ukarabati wenyewe
hauonekani kama umefanyika.
Alisema kitendo hicho
kinapelekea kurudisha nyuma kasi ya maendeleo ya halmashauri hiyo na kueleza
kwa maslahi yake inabidi soko hilo
livunjwe lakini mchakato huo uendane na kuwashirikisha wataalamu ili waweze
kuamua nini kifanyike.
Diwani huyo alisema lazima
madiwani wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wananchi
wanaowaongoza ili kuondoa kero zao lengo likiwa ni kuwapa maendeleo.
“Kila mwaka zilikuwa zikitengwa milioni 50
kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo lakini watu
walikuwa hawazisema ila hizo milioni 11 kwa ajili ya kupewa mtathimini zimekuwa
zikileta maneno naamini wataalamu tunao kwenye halmashauri waamue nini cha
kufanya pale lakini hilo
soko bora livunjwe “Alisema Gadafi.
Akizungumza suala hilo,Mjumbe wa Kamati
wa Fedha,Shehe Fadhili Bwanga alisema
masuala ya kuvunjwa soko hilo ni kutokana na kuona kuwa halikidhi haja ya
kuendana na hadhi ya jiji na wao kupitia kamati ya fedha wameona zifuatwe
sheria za nchi ikiwemo kuthaminiwa na kampuni zinazotambulika kiserikali ili
ziweze kutoa idhini ya uvunjwaji wa jengo hilo.
Bwanga aliongeza kuwa uamuzi
wa kuvunja soko hilo
pia utatokana na gharama zake za sh.milioni 11 lakini sheria za uvunjwaji
zilizowekwa inabidi zifuatwe kabla ya kuachukua maamuzi wa uvunjwaje wake.
Post a Comment