COASTAL UNION WAISHIKISHA ADABU MTIBWA SUGAR,WAICHAPA 3-0
KIKOSI CHA COASTAL UNION KIILICHOICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 3-0 LEO KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI. TANGA |
WACHEZAJI WA MTIBWA SUGAR NA COASTAL UNION WAKISALIMIANA KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO |
WACHEZAJI WAKIINGIA UWANJANI LEO . |
Na Oscar Assenga,Tanga.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga leo wakiwa chini ya
Kocha Joseph Lazaro wamefanikiwa kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 3-0,katika mchezo
wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja w a Mkwakwani mjini hapa.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani
mkubwa ambapo Coastal Union waliweza kuandika bao lao la kwanza kwenye dakika
ya 20 kupitia Crispian Odulla aliyemalizia kazi nzuri iliyofanywa na Haruna
Moshi “Boban’
Baada ya kuingia bao hilo,Coastal Union waliweza
kuendeleza wimbi la mashambulizi langoni mwa Mtibwa Sugar na kufanikiwa
kuongeza bao la pili lililofungwa dakika ya 38 kupitia Jerry Santo kwa njia ya
penati iliyotokana na Keneth Masumbuko wa Coastal Union kuangushwa katika eneo
la hatari na Yusuph Nguya wa Mtibwa Sugar na mwamuzi wa mchezo huo Hashim
Abdallah kuamuru ipigwe penati.
Mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Coastal Union
walikuwa wakiongoza kwa bao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo kipindi cha pili
kilianza kwa kasi kwa kila timu kuingia uwanjani hapo zikiwa na hari mpya baada
ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake.
Wakionekana kujipanga baada ya kufanya mabadiliko
kwa kuwatoa baadhi ya wachezaji wake wakiwemo Dickson Mbeikya na kumuingiza Jamal
Mnyate hali ambaye iliweza kukiongezea nguvu kikosi hicho.
Kutokana na mabadiliko hayo,Mtibwa Sugar waliweza
kujipanga na kupeleka mashambulizi langoni mwa Coastal Union lakini Mlinda
mlango wake,Shabani Kado aliweza kuwa shujaa kwa kupangua mashuti makali ambayo
yalikuwa yakiekezwa langoni lake.
Kwa kuonyesha wao wanacheza kwa umakini
mkubwa,Coastal Union waliweza kubadilisha aina ya mchezo ambao walikuwa
wakioncheza hapo awali na kufanikiwa kulishambulia lango la Mtibwa Sugar kwa
dakika kadhaa na hatimaye Coastal Union kuweza kuhitimisha karamu ya mabao
langoni mwa Mtibwa kupitia Daniel Lyanga baada ya kutokea piga ni kupige
langoni mwa timu hiyo.
Mwisho.
Post a Comment