PINDA KUFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI TANGA ALHAMISI
NA AMINA OMARI,TANGA.
WAZIRI
Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
kongamano la uwekezaji la kanda ya Kaskazini linalotarajiwa kufanyika
Septemba 26 hadi 27 mwaka huu Mkoani Tanga.
Akiongea
na waandishi wa habari hapo leo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa
alisema kuwa waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili Mkoani humo kesho majira ya saa kumi na Moja kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano hilo.
Alisema
kuwa kongamano hilo lenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji na
kimaendeleo zilizoko kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Manyara na Arusha
zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni 450 kutoka nje ya Tanzania.
“Tayari
tumepata wageni wenye nia ya kushiriki ili kujionea fursa zilizopo
takribani 450 wamethibitisha ushiriki wao kutoka nje ya Tanzania
achiambali wale wadau kutoka kwenye Halimashauri zetu mbalimbali zilizoko kwenye ukanda wa kaskazini”alisema RC Gallawa.
Aidha
alieleza kuwa kongamano hilo litakuwa na midahalo ,maonyesho ya
raslimali zilizopo ,maeneo ya uwekezaji pamoja na fursa
zinazopatikananaili kumvutia mwekezaji kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kuichumi kwenye mikoa hiyo.
Pia
aliwataka wakazi wa jiji la Tanga kuhakikisha wanaituma fema fursa ya
uwekezaji hasa kwa wafanyabiashara wa mnumba za kulala wageni na
waendesha biashara za chakula kutoa huduma bora kwa wageni watakao fika
kwa wingi kwenye kongamano hil
Post a Comment