Handeni sasa kujipanga na maabara shule za sekondari
Na Kambi Mbwana, Handeni
MKURUGENZI Mtendaji wilaya Handeni, mkoani Tanga, Khalfany Haule, amesema wanakabiriwa na changamoto ya ukosefu wa maabara kwa shule za sekondari, hivyo wanajipanga kushirikiana na wadau ili kufanyia kazi na kuinusuru elimu wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani, akiwa ofisini kwake.
Akizungumza mjini hapa, Haule alisema maabara hizo ni kwa shule
zote za sekondari zilizopo wilayani humo, jambo ambalo linaweza kuchangia
kufanya vibaya kwa wanafunzi kwenye mitihani ya Taifa.
Alisema anajipanga na watendaji wengine wilayani humo, ikiwa ni
sambamba naa kubuni wazo la kuwashirikisha watu wenye moyo na uwezo wao
kulitatua suala hilo kwa kiasi kikubwa.
"Hapa kuna shule za sekondari ambazo kwa hakika zinafanya
vibaya kwasababu ya ukosefu wa maabara za kuwapa wanafunzi mwanga wa kuendelea
vyema katika masomo yao.
"Lengo ni kuanza kujenga maabara hizo, hivyo tutapenda kushirikiana na wadau wote wenye malengo ya kuinusuru elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaandaliwa vyema,” alisema Haule.
Wilaya ya Handeni ipo chini ya Mkuu wa wilaya wake, Muhingo
Rweyemamu, huku ikifanikiwa na kuwa na mbunge Abdallah Kigoda ambaye pia ni
Waziri wa Viwanda na Biashara.
Post a Comment