Mmarekani mpigania Al shabaab auawa
Wakaazi wa eneo la Gedo Kusini
Magharibi mwa Somalia, wanasema kuwa mwanamgambo wa kiisilamu mwenye
asili ya kimarekani, ameuawa na wanamgambo wa al Shabaab.
Inaarifiwa wawili hao walikuwa wamejitenga na kundi la Al Shabaab . Mwenzao mwenye asili ya Misri alikamatwa.
Kundi la Al Shabaab limekuwa likikumbwa na migawanyiko huku wapiganaji wa kigeni pamoja na wapiganaji wengine wakilengwa na kiongozi wa mwenye msimamo mkali wa Al shabaab Ahmed Abdi Godane.
Godane anaongoza wapiganaji wake katika kupigania wanachokiita taifa la kiisilamu
Post a Comment