Afariki kwa kugongwa na treni Morogoro
Mtu mmoja
amefariki dunia baada ya kugongwa vibaya na treni wakati akivuka reli
na kisha viungo vyake kusambaa katika mtaa wa ujenzi manispaa ya
morogoro .
Wakizungumza
na ITV mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alijulikana kwa jina
moja la mangi ambapo wameeleza kusikitishwa na ajali kwakua hii ni mara
ya tatu watu kugongwa na treni katika maeneo hayo na kueleza kuwa
amarehemu alikua anavuka Reli.
Naye
mwenyekiti wa mtaa wa ujenzi Christopha Chales ameelezea tukio hilo na
kuwataka wananchi kuacha tabia ya kupita kwenye njia ya Reli kwani
wataendelea kusababisha ajali zisizo za lazima ambazo zingeweza
kuepukika.
Askari
wajeshi la polisi wamefika katika eneo la tukio na kuchukua mwili wa
marehemu ambapo umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa morogoro .(KILONGE)
Post a Comment