Mgogoro wa wakazi wa Sarumagaoni Halmashauri ya Jiji la Tanga,
wanaodai kutokana na kuhamishwa katika eneo hilo umeingia katika sura
mpya baada wakazi hao kutishia kuandamana hadi ofisi za mkuu wa mkoa.
Eneo la Sarumagaoni limekuwa katika mgogoro wa muda mrefu pamoja na juhudi kutoka viongozi wa Serikali kujaribu kuutatua.
Mgogoro huo ulipamba moto baada ya kuwepo na
taarifa za kuanza ujenzi wa barabara na reli kwenda Bandari Mpya ya
Mwambani. Wakizungumza katika mkutano wa wananchi jana, wakazi hao
walisema kwamba wamechoshwa na ukimwa wa Serikali hivyo dhamira iliyo
mbele yao kwa sasa ni kufanya maandamano kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Chiku Gallawa.
Weshangazwa na ukimwa wa serikali, kwani mpaka
sasa hakuna tathmini yoyote iliyofanywa jambo ambalo wananchi wanaona
kama vile ni maandalizi ya kunyimwa haki yao.
“Tumeshasema na leo tunafanya hivyo tena,
hatuondoki mpaka haki zetu tuzipate. Hatutaki tathmini ya kutumia
darubini,” walisema zaidi.
“Baada ya kumalizika mkutano huu, tutaunda kamati
ya maandalizi ya maandamano ya amani mpaka kwa Gallawa, tuna imani
polisi wataturuhusu.”
Post a Comment