Featured Post Today
print this page
Latest Post

STAKABADHI GHALANI KITANZI CHA WAKULIMA

STAKABADHI GHALANI KITANZI CHA WAKULIMA


Mkulima wa korosho katika kijiji cha kichonda mkoa wa Mtwara, akipalilia shamba lake.
 
Umasikini umeendelea kuwa kitanzi kwa wakulima wa korosho nchini licha ya mkakati wa kuwakomboa chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani ambao unadhihirika kuwa kero na usumbufu mkubwa kwao.
Mbali ya mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa kero, pia umeamsha uhasama wa kijamii, kulazimisha wanavijiji kuhama makazi yao ya asili na sasa baadhi ya wakazi wa mikoa ya Mtwara na Ruvuma wanaishi kwa majuto.

Mpango wa stakabadhi ghalani kwa wakulima wa korosho unaoratibiwa chini ya Sheria Namba 10 ya Stakabadhi Mazao Ghalani ya mwaka 2005, unathibitika kuwa umeshindwa kuleta matokeo ya kuridhisha chanya kwa wakulima wa korosho.

NIPASHE ilifanya ziara ya uchunguzi wa kihabari kufika kwenye maeneo tofauti yenye wakulima wa korosho hususani Kusini mwa Tanzania.

Unapozungumza nao kuhusu hatima ya maendeleo na uchumi wao unaotegemea korosho, wanaonekana kukata tamaa, wakielekezea kidole kwa serikali kwa kushindwa kuwakomboa, badala yake kuwaacha wakiathiriwa kwa namna tofauti, mojawapo ikiwa ni pamoja na matumizi ya stakabadhi ghalani.

Bodi ya Korosho (CBT) inaeleza kuwa Tanzania ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa zao hilo barani Afrika, ikizalisha wastani wa tani za ujazo 100,000 kwa mwaka.

Mwaka jana pekee, Tanzania ilizalisha tani 127,939.42 za korosho, ikitanguliwa na Nigeria na Ivory Coast. Duniani, Tanzania inashika nafasi ya nane katika uzalishaji wa zao hilo.

Hii ina maana kwamba kama ufanisi katika utekelezaji wa sera, mikakati na mipango inayolihusu zao hilo ingefanikiwa, wakulima wake wangepiga hatua kubwa kiuchumi na nyanja nyingine za maendeleo.

KARAHA ZA STAKABADHI GHALANI
Mfumo wa stakabadhi ghalani ulipoanzishwa msimu wa mwaka 2006/2007 wakulima na wadau wa korosho waliupokea kwa matarajio ya kuwakomboa kiuchumi.

Mfumo huo ulisababisha mkulima kuuza korosho kwenye Ushirika ambao ungemlipa bei ya soko, wakati huo zao hilo likitafutiwa mnunuzi kwa njia ya zabuni, hali ambayo ingesababisha kuwapo kwa malipo ya pili.

Wakati wote huo korosho iliundiwa utaratibu wa kuwekwa kwenye vifaa bora (magunia) na kuhifadhiwa katika maghala ili pamoja na mambo mengine, iwe salama na isipoteze ubora wake.

Hivyo, mkulima alipaswa kugharimia mahitaji hayo ambayo hata hivyo, kutokana na utambulisho ulioonyesha kuwapo manufaa yanayotokana na stakabadhi ghalani, walikubali.

Kabla ya kuanzishwa kwa stakabadhi ghalani, wakulima wa korosho waliuza zao hilo kupitia biashara huria, hivyo kusababisha kupunjwa bei, ingawa walipata fedha kwa wakati. 

Stakabadhi ya mazao ghalani ikaanzishwa kwa mujibu wa Sheria namba 10 ya mwaka 2005, lengo likiwa ni kusaidiana na mifumo mingine ya masoko ili kuwezesha uuzaji wa mazao ya wakulima katika masoko ya ndani na nje.

Wakulima kadhaa wameelezea kutoridhishwa na utekelezaji wa stakabadhi ghalani, kwa madai kuwa licha ya kuwacheleweshea malipo ya awali, hakuna awamu ya pili ya ulipaji fedha za ziada unaofanyika, hivyo kuamini kwamba wananyonywa stahili zao.

Hali hiyo imeibua kundi la wakulima wa korosho wanaoachana na kilimo cha zao hilo na kujishughulisha na mazao ya aina nyingine ikiwamo mpunga.

Mohamed Matoro ni mkulima wa korosho katika kijiji cha Kitanda kilichopo wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, anasema ameamua kuwekeza zaidi katika kilimo cha mpunga na kuachana na korosho.

Kabla ya uamuzi huo, alikuwa anamiliki shamba la korosho lenye ukubwa wa ekari nne. Haikujulikana anamiliki shamba la mpunga lenye ukubwa gani.

“Sijalipwa malipo yangu ya pili kwa mauzo ya msimu wa 2012/13, kwa miaka ya nyuma nililipwa nusunusu, kwa sasa sioni umuhimu wa kuendelea kung’ang’ania zao hili, nimeamua kujaribu maisha katika zao la mpunga,” anasema.

 Matoro ana watoto watano wawili wanasoma katika shule ya msingi Kitanda na watatu wapo nyumbani wameshindwa kuanza elimu ya msingi kutokana na kushindwa kupata fedha zinazokidhi mahitaji ya familia yake.

Wapo wakulima mbalimbali wanaoishuhudia hali kama ya Matoro, wakionekana kukabiliwa na uduni wa maisha unaotokana na kipato kidogo cha korosho ambayo ni zao kuu la biashara kwao.
Wengine miongoni mwa wakulima wa korosho wameamua kujishughulisha na kilimo cha ufuta, wakisema mfumo wa ununuzi wake unaofanyika kati ya mkulima na mfanyabiashara anayelipa fedha kabla ya kuchukua mazao, unawapa uhakika zaidi wa kipato.

Imebainika kwamba licha ya utajiri unaotokana na korosho, wakulima wa zao hilo wana maisha duni yanayowafanya washindwe hata kuchangia huduma za kijamii kwenye maeneo yao.

Mathalani, wakazi wa kijiji cha Azimio wilayani Tunduru, hawana huduma ya maji hususani ya visima, hivyo kusafiri umbali wa kilomita tatu ili kuyafuata.

Maji hayo ya mto Matinjira hayakutegemewa katika miaka ya 1980 kutokana na kuwapo kwa visima vilivyoanzishwa na wahisani, vikasimamiwa, kugharimiwa na kuendeshwa na wakulima, lakini hivi sasa vimekauka.

Sababu ni kushindwa kumudu gharama ya kuviendesha ikiwa ni pamoja na kugharimia utunzaji wa mazingira yanayovizunguka.Si suala la maji pekee, hata wanapohitaji kusafiri, wakulima wengi wa korosho hawawezi kumudu gharama ya safari moja inayotozwa Sh. 2,000, badala yake wanatembea kwa miguu.

Hatua ya wakulima kuachana na korosho imejitokeza katika vijiji vya Kichonda na Mbuli wilayani Liwale katika mkoa wa Lindi ambako sasa wanazalisha mazao mengine yanayohitaji gharama ndogo kuliko ilivyo kwa korosho.

Mustapha Ng’ahama na Kasimu Ngahama ni wakulima wa korosho katika kijiji cha Kichonda, wanasema kilimo cha ufuta kimesababisha baadhi yao (wakulima) kuyahama makazi ya kudumu kwenda kulima ufuta maeneo ya mbali.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Zuberi Mnyuke, anatoa mfano kuwa takribani kaya 150 kati ya 256 zilizopo kijijini humo, zimeyahama makazi yao walipojihusisha na kilimo cha korosho kwenda vijiji vya mbali kulima ufuta.

STAKABADHI GHALANI NA MALIPO DUNI
Hali ya kutoridhishwa na malipo yanayofanywa kupitia stakabadhi ghalani inajitokeza pia kwa wakulima wa maeneo ya Masasi, Liwale, Tambahimba na Newala.

Hoja ya kuwapo manufaa ya ununuzi huru wa korosho uliofanyika kabla ya kuanzishwa kwa stakabadhi ghalani, inaungwa mkono na mkulima wa kijiji cha Ilala wilayani Tandahimba, Rashid Njopa.

Wakulima Hemed Mnukwile wa kijiji cha Mbuli wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi na Ablai Mkuka wa kijiji cha Namiyonga wilaya ya Newala, wanasema gharama za uzalishaji wa korosho ni kubwa kuliko kipato kinachotokana na uuzwaji wake.

Mnukwile mwenye shamba la ekari 24 anaeleza kuwa tangu aanze kulima korosho mwaka 2002, hajaona maendeleo ya maana kutokana na kilimo hicho.

“Desemba mwaka jana nililipwa Sh. 345,000 kama malipo ya awali ya korosho, lakini hadi sasa sijalipwa malipo ya pili yanayofikia Sh. 534,000,” anasema.

Anafafanua kuwa aliuza kilo 879 za korosho huku akitumia gharama ya Sh. 543,000 tangu maandalizi ya shamba hadi mavuno.

Mnukwile anamiliki nyumba anamoishi, ikiwa imejengwa kwa tofali za udongo na kuezekwa mabati yaliyochakaa yakionyesha kutanda kutu huku ikiwa na madirisha yaliyozibwa kwa vipande vya miti na kufunikwa.

Kadhalika kitanda anacholalia kwenye nyumba hiyo ya vyumba viwili anavyovitumia na familia yake ya mke na watoto wawili wanaosoma katika shule ya msingi Mbuli, kimesokotwa kwa kamba za katani.

Naye mkulima Mkuka mwenye shamba la ekari 20, anasema Desemba mwaka jana alivuna kilo 3,500 za korosho zenye thamani ya Sh. 3,500,000, lakini aliambulia Sh. 650,000 kwa malipo ya awali.

Anasema hadi kufikia Februari mwaka huu, alikuwa hajalipwa fedha zilizobaki, huku akitaja gharama alizozitumia kwa kilimo zilifikia Sh. 932,500.

Hali ya kimaisha ya Mkuka ni duni, ikithibitika kwa kuishi kwenye nyumba ‘iliyochoka’ huku akishindwa kununua chakula cha kuhifadhi kwa ajili ya familia yake.

Mkulima mwingine, Ally Kamkole anakidai chama cha msingi cha kijiji cha Azimio Sh. 212,100. Alipata malipo ya awali ya Sh. 515,100 kutokana na kuuza kilo 606 za korosho.  Gharama za uzalishaji wake zilikuwa Sh. 312,000.

Naye Abdallah Haji anakidai chama cha msingi Shilingi 907,900 tangu Desemba 22, 2011. Alipata malipo ya awali ya Sh. 2,204,900, kutokana na kuuza kilo 2,594, bei ya kilo moja ikiwa ni Sh. 1,200.

Wakulima hao kwa nyakati tofauti, wanasema Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Chande Nalicho, aliwatangazia wakulima kuwa hawatalipwa malipo hayo kutokana na mauzo kufanyika kwa hasara.

Hata hivyo, Nalicho alipofuatwa kulielezea suala hilo, alisema: “Kwa sasa sina muda, ninaenda kwenye maafa, nenda kwa Mkurugenzi wa wilaya atakupa majibu.”

Mkurugenzi wa wilaya hiyo aliielekeza NIPASHE ionane na Ofisa Kilimo Msaidizi Mkuu wa Tunduru, Fidelis Francis Nyakunga.
Nyakunga anakana na kusema: “Si kweli mkuu wa wilaya aliwatangazia wakulima kuwa hawatapata malipo yao ya pili.”

VIONGOZI: MAZINGIRA DUNI YANAKWAMISHA KILIMO CHA KOROSHO
Viongozi kadhaa wa serikali, wanathibitisha kuwapo mazingira yanayokwamisha ustawi wa wakulima wa korosho, hivyo kufifisha jitihada za kuliboresha zao hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Ephraim Mmbaga, anasema wapo wakulima wa korosho wanaoyahama makazi yao kwenda vijiji vya mbali kulima ufuta, wakiachana na kilimo cha korosho.

Mmbaga anasema miongoni mwa sababu zinazotajwa kwa ushawishi huo ni mazingira duni kwa kilimo cha korosho wakati zao kama ufuta, halihitaji gharama kubwa katika maandalizi, kulima na uvunaji wake.

Kwa mfano, anasema bei ya ufuta kwa msimu uliopita ilikuwa kati ya Sh. 2,000 hadi 2,800 kwa kilo moja, fedha zinazolipwa pasipo makato ama gharama kama zinazotozwa kupitia stakabadhi ghalani.

Pia Mmbaga anasema ufanisi duni wa mfumo wa stakabadhi ghalani unachangiwa na hujuma zinazofanywa na baadhi ya watendaji serikalini, lakini hawataji majina.

“Watendaji wachache wanatokea na kuwaibia wakulima, mfumo wenyewe ni mkombozi wa wakulima, hivyo hauna tatizo, tatizo ni watendaji,” anasema Mmbaga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Farida Mgomi anasema stakabadhi ghalani bado haijaeleweka vizuri kwa wakulima na kwamba wengi wao (wakulima) wanadhani kuwa unawanyonya.

“Kinacholeta msuguano juu ya mfumo wa stakabadhi ghalani ni elimu ndogo waliyonayo wakulima, pamoja na hatua ya ukopaji wa vyama vya ushirika katika benki,” anasema.

 Anasema moja ya sababu zinazochochea uelewa duni ni kushindwa kwa maofisa ugani kuwatembelea wakulima vijijini.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kichonda, Mnyuke anasema robo tatu (sawa na watu 264) ya wakazi wa Kichonda wanaokadiriwa kuwa 350 ‘wamekimbilia’ katika vijiji vya Milui, Kiangale, Kipelele, Naujombo, Kimumbi, Zinga, Likawage na Nanjilinji ili kushiriki kilimo cha ufuta.
CHANZO: NIPASHE
0 comments

MATANGAZO YA WAGANGA WA JADI YAMKERA MKUU WA WILAYA YA TANGA


MATANGAZO YA WAGANGA WA JADI YAMKERA MKUU WA WILAYA YA TANGA







MATANGAZO ya waganga wa jadi wanaotibu ukimwi kwa dawa za asili, yanawavunja moyo watafiti na wanasayansi wanaoendelea kutafuta tiba ya ugonjwa huo.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto uliofanyika viwanja vya Tangamano jijini hapa.
Alisema matangazo hayo yanawatia hofu wananchi na kuamini kuwa serikali na wataalamu wa afya wameshindwa kutafuta tiba ya ugonjwa huo huku yakichochea ngono.
“Tatizo hili limechangia kuongezeka kwa waathirika wengi wa ukimwi… iwapo hatutachukua hatua za kudhibiti kwa haraka, kuna uwezekano wa serikali kushindwa kuwahudumia waathirika wa ungonjwa huo,” alisema.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Asha Mahita, alisema ni asilimia 21.9 ya wanaume ndio wanaohudhuria kliniki wakiongozana na wenza wao kwa ajili ya kupima virusi vya ugonjwa huo hali inayoonyesha kuwa jamii inahitaji msukumo katika hili.
“Natumia fursa hii kuwaomba waheshimiwa madiwani watusaidie kuhamasisha wananchi wote kupima virusi vya ukimwi kwa hiari kwa kuwa sasa hivi mtazamo ni afya chanya na kinga kwa sababu huduma za dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo zinapatikana kwa urahisi kwenye vituo vya afya,” alisema Dk. Mahita.
Chanzo;Tanznia Daima 
0 comments

LOGARUSIC MENO NJE BAADA YA KUSIKIA PANDE LA AVEVA



Kocha Zdravko Logarusic amefurahia kusikia mmoja wa wagombea wa urais Evans Aveva akisema wataendelea kufanya naye kazi.
Logarusic ambaye yuko mapumzikoni kwao Croatia amesema bado ameelekeza nguvu zake Simba, hivyo amejisikia vizuri kwamba hafanyi kosa kuendelea kusubiri.

“Nimepata ofa mara mbili lakini bado niliendelea kusubiri Simba wamalize uchaguzi. Sasa nimesikia hata wagombea wa urais wamesema wanatafanya kazi na mimi.

“Nimesoma kwenye mitandao, jambo zuri kwangu na inanipa moyo wa kufanya kazi kwa juhudi zaidi nitakaporejea.

“Unajua mtu akionyesha kukuamini ni deni kubwa kwao, hii ndiyo ipo kwangu. Lakini sina hofu na Simba msimu ujao kuwa itafanya vizuri,” alisema Logarusic.

Logarusic ndiye alikuwa kocha wa Simba kwa nusu msimu akichukua nafasi ya Abdallah Kibadeni aliyeanza nayo msimu.
0 comments

CHEKI MAPICHA MAXIMO ALIVYOTUA KWA KISHINDO DAR ES SALAAM


MAXIMO AKIWASALIMU MASHABIKI WA YANGA.



WATU KIBAO


0 comments

MAXIMO NDANI YA DAR, YANGA RAHA TUPU

MAXIMO NDANI YA DAR, YANGA RAHA TUPU

Kocha mpya wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo kushoto baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mchana huu tayari kuanza kazi. (Picha zaidi zitafuatai).
0 comments

KAZI IMEANZA, SIMBA SC YASAINI BEKI LA TAIFA STARS MIAKA MITATU...YANGA NA MAGAZETI YAO

KAZI IMEANZA, SIMBA SC YASAINI BEKI LA TAIFA STARS MIAKA MITATU...YANGA NA MAGAZETI YAO

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KAZI imeanza. Simba SC imesajili mchezaji wa kwanza kabisa kwa ajili ya msimu ujao, ambaye ni chipukizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Joram Nason Mgeveke.
Mchezaji huyo chipukizi pekee kutoka kikosi cha maboresho aliyebaki Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij, amesaini Mkataba wa miaka mitatu leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Joram amesaini mjini Iringa na rasmi sasa ni mchezaji wa Simba SC.

Kifaa cha kwanza 2014-2015; Joram Mgeveke akipeana mikono na Hans Poppe baada ya kusiani Mkataba wa miaka mitatu na Simba SC. Chini anasaini.


“Tuna muda mfupi sana kwa ajili ya kufanya usajili, sasa tuna orodha ya wachezaji waliopendekezwa, kwa hiyo tunaanza kuwapandia ndege kuwafuata na kumalizana nao, ndani na nje ya nchi. Tumeanza na Joram, kwa sababu yuko Taifa Stars ambayo inakwenda kambini Botswana,”alisema Poppe.   
Poppe amewahakikishia wana Simba SC kwamba safari hii watasajili wachezaji bora ambao watarejesha heshima ya klabu hiyo msimu ujao.
Kwa upande wake, beki huyo mwenye misuli anayecheza nafasi za kati za ulinzi, amesema kwamba amefurahi mno kujiunga na Simba SC kwa sababu ni timu kubwa, ambayo anaamini itainua kiwango chake na kumfungulia milango zaidi ya mafanikio.
Joram Mgeveke wa pili kutoka kushoto waliosimama akiwa kikosini Stars dhidi ya Malawi

“Kwa kweli nimefurahi sana kujiunga na Simba SC, ni timu kubwa na ya kihistoria hapa Tanzania ambayo wamepita wachezaji wengi wazuri, ambao na mimi ningependea kufuata nyayo zao,”amesema.
Beki huyo alicheza kwa dakika 75 mechi ya kirafiki ya Tanzania na Malawi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo bao pekee la Amri Kiemba wa Simba SC liliipa Taifa Stars ushindi wa 1-0 kabla ya kumpisha Kevin Yondan wa Yanga.
Tangu hapo amekuwemo kwenye orodha ya wachezaji 18 walioshiriki mechi zote za Stars dhidi ya Zimbabwe kufuzu Mataifa ya Afrika kama mchezaji wa akiba.
Nyota Njema ndiyo iliyomuibua kinda huyo mwenye umri wa miaka 22, baadaye akachezea Polisi na Lipuli zote za Iringa, kabla ya kuchukuliwa timu ya mkoa, ambayo ilimfungulia milango ya kuingia Taifa Stars kupitia mpango wa maboresho. Katibu wa Lipuli, Willy Chikweo ametoa baraka zake zote juu ya usajili huo. “Kuanzia sasa, Joram ni wa Simba SC, kwa roho safi kabisa na tunamtakia kila la heri,”amesema katibu huyo.
Wakati Simba SC inafanikisha usajili wa mchezaji wa kwanza wa msimu ujao, watani wa jadi Yanga SC wanaendelea kupamba kurasa za magazeti kwa majina ya wachezaji tofauti ambao inadaiwa wanataka kuwasajili kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Na wakati dirisha la usajili linafungwa mwishoni mwa mwezi huu, hakuna mchezaji hata mmoja ambaye hadi asa Yanga SC imesema rasmi imemsainisha Mkataba, huku ikiwa tayari imewapoteza Frank Domayo na Mrundi Didier Kavumbangu waliohamia Azam FC.
0 comments

MGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI



Mbunge wa  jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura wake katika kijiji cha Kivalali kata ya Ifunda baada ya gari lake  kupata pacha  wakati wa ziara hiyo hivyo kulazimika kutafuta baiskeli ili kufika haraka mkutanoni kusikiliza kero za  wananchi wake.(picha na Francis Godwin Blog) (P.T)
0 comments

KIINGLISHI KILIVYOWAGOMBANISHA ASKARI POLISI NA ASKARI WA MANISPAA YA MOSHI

KIINGLISHI KILIVYOWAGOMBANISHA ASKARI POLISI NA ASKARI WA MANISPAA YA MOSHI

Baada ya kuzunguka kwa muda mrefu raia huyu wa kigeni ambaye haikufahamika mara moja anatoka nchi gani aliketi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kisha akatoa Mkate huku akiulainisha na Jam na kuanza kula.
Alikula Silesi kadhaa lakini alionekana mwingi wa mawazo kila alipotafuna mkate .
Baadae akasukumia mkate na Maji ya Kilimanjaro.
Akafunga maji yake akayarudisha ndani ya begi lake.
Akaendelea kutafuna Mkate.
Akamuuliza mtu aliyekuwa jirani yake vipi unahitaji na wewe nikupatie kidogo na hii ilikuwa ni silesi ya mwisho.
Baada ya kupita muda mgeni huyo aliamua kuondoka eneo alilokuwa ameketi akipata mkate wake wa kila siku.
Ghafla nyuma yake akajitokeza askari wa manispaa ya Moshi (Mwenye t-shirt nyeupe) ambaye ana jukumu la kusimamia maswala ya mazingira.
Baada ya kufuatilia kwa kina ,ikagundulika kuwa askari huyo alikuwa anamfuatilia mgeni huyo akitaka kumtia mikononi kwa kosa la kutupa taka ambazo ni vipande vya mikate na kopo la Jam na kama unavyofahamu sheria za usafi kwa manispaa yetu ya Moshi.
Globu ya jamii ikabahatika kuona vipande vya mikate lakini ilipomuuliza askari huyo ni vipi mbona hajamkamata na kumpeleka kunako husika kama wafanyavyo kwa wabongo wenzao ,askari huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisema anataka kumkamata lakini hawaelewani lugha huku akidai kuwa yeye kimombo hakipandi akalazimika kwenda kuomba msaada kwa asakri polisi kata aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi.
Raia huyo wa kigeni akaondoka zake.
Kumbe askari yule wa mazingira aliyeenda kuomba msaada kwa askari polisi aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi alikutana na zahama nyingine wakati akiomba msaada kwa askari huyu anayeonekana hapa ya kupigwa makofi kwa madai aligoma kwenda kutoa msaada wa kumkamata yule raia wa kigeni kwa kuwa hajui "Kizungu",na hapa askari huyo aliamua kumueleza mwenzake (mwenye t-shirt nyeupe)aliyetambulika kwa jina la Mkude kuhusu tukio hilo ndipo Mkude kwa ghadhabu ya hali ya juu akaenda kuwakamata askari hao wa mazingira.
Wakati asakari hao wa mazingira wakifanya utaratibu wa kumakamata raia huyo wa kigeni ghafla walidakwa na Mkude wote wawili .
Kisha safari ya kwenda Kituoni ikaanza.
Ghafla Mkude baada ya kuona kamera ya globu ya jamii inammulika alimuamuru askari mwenzake kuikamata ,alakini hata hivyo askari yule alifahamu kuwa Globu ya jamii pia iko kazini kama walivyo wao.
Mzobe mzobe ukaendelea kupita katikati ya kituo kikuu cha mabasi huku mbinje za kutosha toka kwa wakatisha tiketi na wapiga debe zikirindima.
Askari Polisi.Mkude akafanikiwa kuwatia mikononi askari wa manispaa ya Moshi wanaoshughulika na mazingira hadi kituoni.Globu ya jamii ilifika hadi kituoni licha ya kwamba asakri wa kata aliyekuwa amevalia sare kudai kuwa yeye aliwasamehe lakini Mkude akiwa kituoni alisimamia msimamo wa kufunguliwa kwa kesi dhidi ya sakari hao.Hata hivyo baadae raia wa kigeni alionekana katika eneo la stendi akiranda randa.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
0 comments

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOANGUSHA BONGE LA KAMUZI JIJINI BRUSSEL

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOANGUSHA BONGE LA KAMUZI JIJINI BRUSSEL

 Diamond Platnumz akifanya mavituzz ukumbini na wacheza show wake wakiwa wanaendeleza manjonjo
 Waaaawwwoohh..ni umati haswaaa..kweli Diamond anapedwa
 Diamond Platnuz kijana mdogo mwenye mafanikio katika mziki na kimaisha akiimba wimbo wa nimpende nani
 V.I.P. table ilijumlishwa na viongozi mbalimbali,pichani ni mke wa Mh: wa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi bwana Kamala aliyevalia nguo ya mizungo miyeusi na miyeupe
 Hapo sasa..Diamond Plutnumz akiendelea kukonga nyoyo za waliofika kumshughudia show yake
 Sema naeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..!! warembo toka Tz wakishangilia show ya Diamond ikiendelea.
                                                              OOOooyoooooooooooh
 Ooooooiiihhh!!! Ni peace n' Love toka kwa watoto wa nyumbani
 Umati wa watu wakiendelea kupata burudani ya muziki toka kwa msanii Diamond Platnumz
Ngololo aai ngololo mama  ngololo...... and show me how they do ngololo ngololo ni Saidi Biboze na dada yake Zuhra Biboze wakijiachia kwa raha zao.
 (Picha zote na Maganga One Blogger)
 (Picha zote na Maganga One Blogger)
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger