KIINGLISHI KILIVYOWAGOMBANISHA ASKARI POLISI NA ASKARI WA MANISPAA YA MOSHI
Baada
ya kuzunguka kwa muda mrefu raia huyu wa kigeni ambaye haikufahamika
mara moja anatoka nchi gani aliketi katika kituo kikuu cha mabasi mjini
Moshi kisha akatoa Mkate huku akiulainisha na Jam na kuanza kula.
|
Alikula Silesi kadhaa lakini alionekana mwingi wa mawazo kila alipotafuna mkate .
|
Baadae akasukumia mkate na Maji ya Kilimanjaro.
|
Akafunga maji yake akayarudisha ndani ya begi lake.
|
Akaendelea kutafuna Mkate.
|
Akamuuliza mtu aliyekuwa jirani yake vipi unahitaji na wewe nikupatie kidogo na hii ilikuwa ni silesi ya mwisho.
|
Baada ya kupita muda mgeni huyo aliamua kuondoka eneo alilokuwa ameketi akipata mkate wake wa kila siku.
|
Ghafla
nyuma yake akajitokeza askari wa manispaa ya Moshi (Mwenye t-shirt
nyeupe) ambaye ana jukumu la kusimamia maswala ya mazingira.
|
Baada
ya kufuatilia kwa kina ,ikagundulika kuwa askari huyo alikuwa
anamfuatilia mgeni huyo akitaka kumtia mikononi kwa kosa la kutupa taka
ambazo ni vipande vya mikate na kopo la Jam na kama unavyofahamu sheria
za usafi kwa manispaa yetu ya Moshi.
|
Globu
ya jamii ikabahatika kuona vipande vya mikate lakini ilipomuuliza
askari huyo ni vipi mbona hajamkamata na kumpeleka kunako husika kama
wafanyavyo kwa wabongo wenzao ,askari huyo ambaye jina lake
halikufahamika mara moja alisema anataka kumkamata lakini hawaelewani
lugha huku akidai kuwa yeye kimombo hakipandi akalazimika kwenda kuomba
msaada kwa asakri polisi kata aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi.
|
Raia huyo wa kigeni akaondoka zake.
|
Kumbe
askari yule wa mazingira aliyeenda kuomba msaada kwa askari polisi
aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi alikutana na zahama nyingine
wakati akiomba msaada kwa askari huyu anayeonekana hapa ya kupigwa
makofi kwa madai aligoma kwenda kutoa msaada wa kumkamata yule raia wa
kigeni kwa kuwa hajui "Kizungu",na hapa askari huyo aliamua kumueleza
mwenzake (mwenye t-shirt nyeupe)aliyetambulika kwa jina la Mkude kuhusu
tukio hilo ndipo Mkude kwa ghadhabu ya hali ya juu akaenda kuwakamata
askari hao wa mazingira.
|
Wakati asakari hao wa mazingira wakifanya utaratibu wa kumakamata raia huyo wa kigeni ghafla walidakwa na Mkude wote wawili .
|
Kisha safari ya kwenda Kituoni ikaanza.
|
Ghafla
Mkude baada ya kuona kamera ya globu ya jamii inammulika alimuamuru
askari mwenzake kuikamata ,alakini hata hivyo askari yule alifahamu kuwa
Globu ya jamii pia iko kazini kama walivyo wao.
|
Mzobe
mzobe ukaendelea kupita katikati ya kituo kikuu cha mabasi huku mbinje
za kutosha toka kwa wakatisha tiketi na wapiga debe zikirindima.
|
Askari
Polisi.Mkude akafanikiwa kuwatia mikononi askari wa manispaa ya Moshi
wanaoshughulika na mazingira hadi kituoni.Globu ya jamii ilifika hadi
kituoni licha ya kwamba asakri wa kata aliyekuwa amevalia sare kudai
kuwa yeye aliwasamehe lakini Mkude akiwa kituoni alisimamia msimamo wa
kufunguliwa kwa kesi dhidi ya sakari hao.Hata hivyo baadae raia wa
kigeni alionekana katika eneo la stendi akiranda randa.Na Dixon Busagaga
wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
|
Post a Comment