Featured Post Today
print this page
Latest Post

WANANCHI WA MJI KOROGWE WAUPOKEA KWA KISHINDO MPANGO WA TIKA, WACHANGIA MIL. 1.3

WANANCHI WA MJI KOROGWE WAUPOKEA KWA KISHINDO MPANGO WA TIKA, WACHANGIA MIL. 1.3


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa (kushoto). Pembeni ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Singida, Bw. Issaya Shekifu akitoa uzoefu wake katika moja ya Wilaya ya Ilamba, Singida jinsi wananchi wanavyofaidika na TIKA.
Viongozi wa Dini wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Msikiti Mkuu Manundu, Korogwe Mzee Daffa Daffa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akisalimia na viongozi wa dini wa Halmashauri ya Mji Korogwe mara baada ya kumaliza kufungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Waheshimiwa Madiwani wa Kata mbalimbali za Halmshauri ya Mji Korogwe wakiwa katika mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
NHIF 11: Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)- Dar es Salaam, Genoveva Vicent akitoa majumuisho jinsi Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) unavyoweza kuwasaidia wananchi.

 Mchungaji Joseph Mhina wa Kanisa la Anglikana Manundu, Korogwe akitoa shukrani kwa wananchi waliofika katika mkutano huo wa wadau. 
Timu ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dar es Salaam na Tanga waliokuwa wakiratibu mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa na Wilaya. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
0 comments

Utapiamlo; tatizo sugu linalotesa wengi Kilindi

Utapiamlo; tatizo sugu linalotesa wengi Kilindi

 
 Makombo Hatibu  akimlisha uji wa lishe mtoto Hatibu Abdallah, kushoto ni mtoto Asha Abdalah hivi karibuni mkoani Tanga
Kwenye duka mojawapo lililopo katika eneo la Mgera wilayani Kilindi mkoani Tanga, nakutana na mama mwenye mawazo mengi, mkononi amewapakata watoto wawili ambao wanalia muda wote.
Mmoja wao ana tumbo kubwa na mwingine amepauka uso, nywele zimelainika kwa kiasi kikubwa.Hali ile ilinishtua na kunilazimu nimsogelee mama yule ili kujua tatizo gani linalomsumbua yeye na watoto wake.
Kwa upole alinijibu kwa kuanza kunieleza kuwa watoto wake wanalia kutokana na njaa na kwamba wanakula mlo mmoja na nyakati za asubuhi anawalisha viporo
Mama huyo, Mwamvua Bakari anasema watoto wake wamegundulika kuwa na utapiamlo baada ya Kikundi cha Afya na Lishe, Mama Mjamzito na Mtoto kilichopo Mgera kumtembelea nyumbani kwake na kubaini watoto wake wanalo tatizo hilo.
Hayuko peke yake, wapo kinamama na watoto wengi zaidi wenye tatizo kama hilo wilayani Kilindi na Mkoa wa Tanga kwa jumla.
Hata hivyo, serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali za huduma ya afya, mama na mtoto kupitia Shirika la World Vision wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa tatizo hilo linapungua nchini.
Kutokana na jitihada hizo, wameweza kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaokufa kwa utapiamlo nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Mwanamvua kwa upande wake anaeleza kuwa kuanzia mwaka 2010 wakati alipojifungua mtoto wake wa kwanza maisha yake yalikuwa magumu kutokana na umaskini unaoikabili familia yao.
Anasema mume wake amekuwa akitegemea zaidi vibarua vya kulima ili apate fedha ya kununulia walau kibaba cha unga na wakati mwingine hulazimika kulala na njaa.
“Tatizo kubwa ni kuwa mimi na mume wangu hatuna kipato, hivyo nilianza kuwaacha watoto wa miezi tisa nyumbani bila chakula. Kwa sasa, mmoja ana miaka mitatu na mwingine mitano, wote nilikuwa nikiwaacha kwa bibi yao nao walikuwa wanakunywa uji asubuhi hadi jioni tutakaporudi kutoka kwenye mahangaiko,” anasema.
Anaeleza kuwa maisha yao yalipokuwa magumu zaidi, walilazimika kununua nusu kilo ya unga ambao haukutosha, kiasi kwamba walikula mlo mmoja kwa siku na kulazimika kuacha kiporo ili watoto wanapoamka asubuhi waweze kula.
Baada ya kikundi hicho kuwatembelea nyumbani kwao walimweleza aende kliniki kwa ajili ya kupima uzito wa watoto hao. Mtoto wa miaka mitatu alikutwa na uzito wa kilo 11.3 na yule mwenye miaka mitano akiwa nazo kilo 10.3 pia.
Mama mwingine mwenye watoto pacha wenye miaka miwili aliyejitambulisha kwa jina la Makombo Hatibu anasema watoto wake aliwaanza kula kiporo cha ugali wakiwa na umri wa miezi sita.
Anasema inategemea siku hiyo kama unga umebaki kidogo anawapikia uji kama hakuna siku hiyo analazimika kumsubiri mume wake hadi hapo atakaporudi jioni ili wapike chakula.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Afya ya Lishe, Mama Mjamzito, Muya Atanasia anasema waliwabaini watoto hao wakati wanapita nyumba kwa nyumba wakitoa elimu ya lishe.
Anasema baadaye waliwachukua wazazi hao kwa ajili ya kutoa elimu ya lishe bora ili waweze kujifunza jinsi ya kutengeneza lishe isiyokuwa na gharama kwa kutumia mazao wanayolima kijijini hapo.
Anaelezea kikundi chao kinawakusanya watoto wote waliopata utapiamlo kwa kuwapikia uji wa lishe uliochanganywa na karanga, mchele, ulezi na maharage wakati huo wanawaelekeza wazazi wao jinsi ya kuandaa vyakula hivyo.
“Baada ya kunywa uji huo tunawapa tunda huku uji mwingine tunawaelekeza wazazi wao waweke kwenye chupa kama chakula kimechelewa ili waweze kunywa.
“Kwa kupunguza gharama ya ulezi, mara nyingi tunawashauri jamii watumie mahindi ya lishe yaliyochanganywa na maziwa kwa ajili ya kupunguza gharama kulingana na maisha wanayoishi kijijini huku,”anasema.
Anaongeza kuwa mara nyingi wanaelekezwa kutumia vipimo zaidi wakati huo wakisisitiza uji huo unapoandaliwa unawekwa sukari na chumvi wakati wa kuandaa lishe ya watoto hao.
Anaeleza kuwa watoto hawapati muda mzuri wa kunyonya, hivyo wazazi wao walikuwa hawatambui kuwa viporo kwa mtoto chini ya umri wa miaka mitano husababisha utapiamlo.
Hawazingatii muda wa kula. Wanakwenda shamba na wanaporudi jioni ndipo huandaa chakula cha watu wazima na kuwapa watoto wao bila kujali muda.
“Chakula kikuu wanachopikiwa watoto hao ni ugali na mlenda na baadaye huwaacha watoto wenyewe wale wenyewe. Kwa mfano kama watoto hawa wawili pacha tumewakuta katika hali mbaya ,” anasema mratibu huyo.
Katibu wa kikundi hicho, Mwajabu Mrisho anasema ndani ya siku saba watoto hao waliongezeka uzito. Yule mwenye miaka mitano aliyekuwa na kilo 10.3, aliongezeka na kufikia kilo 11.9 huku mwenye miaka mitatu aliyekuwa na kilo 11.3 hakuongezeka uzito kwa sababu alikuwa na minyoo pamoja na malaria.
Anasema kwa watoto wale pacha, yule wa kike alikuwa na uzito wa kilo 6.5 aliongezeka na kufikia kilo 7.1 na yule wa kiume aliyekuwa na kilo 5.9 aliongezeka na kuwa na kilo 6.8.
Mwajabu anasema wamefanikiwa kutoa elimu ya afya ya mama mjamzito na mtoto, hivyo kutokana na elimu hiyo wanaume wameanza kuwasindikiza wake zao hadi vituo vya afya na hata kujaribu kuwashawishi wake zao kuhudhuria kwenye kliniki mara kwa mara.
Mpango wao kwa mwezi Desemba mwaka huu utatoa elimu katika vijiji vya Jungu, Makingo, Kwendiswati pamoja na Lekiting’e ambapo awamu ya kwanza elimu hiyo ilitolewa kwenye vijiji vya Mgera, Balang’a na Kisangasa na kwamba uhamasishaji utaongezeka.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kata ya Kibirashi, Augustino Semzige anasema kupitia mradi huo, umesaidia kupunguza ugonjwa huo kwa asilimia 75. Miaka ya nyuma uliongezeka kwa asilimia 95 kwa sababu ilitokea njaa kubwa wilayani hapo.
“Mradi huu wa Afya, Mama na Mtoto iongeze nguvu kwa suala la utapiamlo, hasa kuielimisha jamii ili waweze kujua jinsi ya kuandaa lishe ya mama mjamzito na mtoto. Kama mama mjamzito akikosa virutubisho wakati wa mimba anaweza kupata upungufu wa damu na kusababisha kuvimba miguu na uso ambapo anakuwa hana nguvu ya kumsukuma mtoto wakati wa kujifungua,” anasema Dk Semzige
Pia, ushiriki wa wanaume kupitia mradi huo umesaidia kwa asilimia 95 walioanza kuhudhuria kliniki wakiwa na wake zao. Hivyo mwanamume anapogundua kuwa mke au mama ana matatizo, anakuwa mstari wa mbele kumpeleka kwenye kituo cha afya.
Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Wilayani Kilindi, Ruth Ligubi anasema zaidi ya wanaume 6,197 wamekuwa wakishirikiana na wake zao baada ya kupata elimu ya lishe kwa mama mjamzito na mtoto. Kupitia mradi huo, huwajali familia zao na kuzipa kipaumbele lishe bora na kumjali mama mjamzito.
“Wanaume waliokuja na wake zao kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2013 walikuwa 6,197 ukilinganisha na miaka ya nyuma walipokuwa hawazidi 30. Hivyo kwa sasa uelewa umekuwa mkubwa,” anasema.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Dk Shemdaa Ngereza anasema tatizo la utapiamlo ni kubwa hasa kwenye maeneo ya vijiji vya ndani kutokana na kipato kidogo cha fedha cha kuandaa lishe.
Anasema asilimia 4.5 ya watoto waliougua utapiamlo, imepungua kutokana na elimu inayotolewa na mradi wa Afya, Mama na Mtoto kupitia World Vision.
Chanzo;Mwananchi
0 comments

MACHANGU:WABUNGE WAKATIBA WANALIPA VIZURI.


MACHANGU:WABUNGE WAKATIBA WANALIPA VIZURI.


Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini Dodoma wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri.


Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa pesa ndogo wanapowaopoa.

“Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako! Wanalipa vizuri ile mbaya.

“Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au 20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo, tusipojenga safari hii basi tena,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha biashara ni eneo Chako ni Chako.

Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: “Unajua hii biashara inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba ndogo zao kabisa.”

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo sasa imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.

Mwandishi wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako, Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.

Gazeti hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.


Credit:Gazeti la Ijumaa.
0 comments

JINI KABULA AFUNGUKA NA KUSEMA MEMBER WA BONGO MOVIE WENGI NI WAATHIRIKA.


JINI KABULA AFUNGUKA NA KUSEMA MEMBER WA BONGO MOVIE WENGI NI WAATHIRIKA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifwi8N-mnfgUB8FWcyBK9iQRPo13dSsUjcT3OwfEnWKMC88ta-_Kt2eH19YvKWzCy54ImExDeQOW7xETd5m23B3xQnDajA3KAGXmqoJzOhFPeQ3r-Mj9tr9lUjb-0k_I3lbuIYujbbSt4/s640/Miriam-Jolwa-Kabula-cut.jpgKatika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua msanii mkongwe kiwanda cha Bongo movie nchini Miliamu Jolwa maarufu kama Jini Kabula ameibuka na kusema kuwa hakika gonjwa hatari la ukimwi litawateketeza wasanii wote wa Bongo movie na hakuna atakaebaki kama hawatobadilika kitabia.

Akiongea na gazeti la pendwa na Watanzania Maskani Bongo alisem" Sio siri kwa mfano leo hii wasanii wote bongo movie waseme wakamatwe kinguvu wakapimwe HIV utaona hali ilivyokuwa mbaya na sijui hata mmoja atakuwa mzima na sababu kubwa ni njaa ambapo sisi wengi wetu tuna majina lakini hatuna kitu hivyo hiyo hutoa nafasi ya kujirahisha ili kupata pesa" Alisem Kabula kwa uchungu.
0 comments

JOHARI AFUNGUKA NA KUSEMA HATOACHA KUNYWA POMBE HADI MWISHO WA MAISHA YAKE.


JOHARI AFUNGUKA NA KUSEMA HATOACHA KUNYWA POMBE HADI MWISHO WA MAISHA YAKE.


Staa wa bongo movie nchini Johari amefunguka kuwa starehe ya pombe ni sehemu ya maisha yake hivyo kamwe hatoweza kuiacha hadi mwisho wa maisha yake kwa vile hana starehe nyingine aipendayo kama hiyo.
Johari aliongeza kusema katika maisha yake amejilaumu sana kwa nini alichelewa kuanza kutumia pombe kwani ina flava za ajabu ambazo humfanya kusahau shida zake zote na kujikuta yuko sayari nyingine.
CREDIT: MASKANI BONGO.
0 comments

Hati za Muungano mvurugano

Hati za Muungano mvurugano


Utata umezidi kuibuka katika Bunge Maalumu la Katiba kutokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.

Utata huo, umebainika katika Kamati kadhaa siku moja tangu wajumbe wa Bunge hilo waanze kujadili sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.

Jana Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa.
Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UN na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.

Nahodha alisema baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.

Kauli hiyo ya Nahodha inapingana na kauli ya Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad ambaye jana alisema hati hiyo ipo Dar es Salaam na ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.

"Ile hati ya Muungano ipo Dar es Salaam, lakini tunahofia kuileta maana inaweza kupotea kwani ipo moja tu, sasa ambacho tutakifanya inaweza kutolewa nakala na kuthibitishwa na mawakili na ikaja nakala hapa Dodoma iwapo wajumbe wanahitaji," alisema Hamad.

Nahodha alipoelezwa juu ya majibu ya Katibu wa Bunge kuwa hati hiyo ipo Dar es Salaam, alishikwa na mshangao na kusema wanamuomba Katibu huyo, aiwasilishe kama ipo.
Sheria za Muungano.

Katika hatua nyingine, Sheria Namba 22 ya 1964 ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuridhia Muungano nayo haijulikani ilipo.

Baadhi ya wajumbe katika Kamati Namba 2 walidokeza kuwa, walipohoji kuhusu sheria hiyo walisomewa kitabu cha aliyewahi kuwa Mwanasheria wa Zanzibar, Abdul Jumbe na kuambiwa kwamba picha za ukumbusho zipo.

Nahodha ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, alikiri kuwa hata yeye hajawahi kuona sheria hiyo.
"Kwa Bunge la Tanganyika ushahidi tumeletewa hapa kuwa waliridhia Aprili 25, 1964 na waliosaini ni Julius Nyerere, Katibu wa Bunge hilo, Pius Msekwa na aliyekuwa Spika Adam Sapi Mkwawa, lakini kwa Zanzibar haupo," alisema na kuongeza:
"Mimi nilikuwa mtendaji mkuu wa SMZ nilipaswa kujua, lakini nisingeweza tu kuanza kutafuta sheria, sheria ambazo zimetungwa Zanzibar ni nyingi, kwani ingeniwia kazi kubwa sana kuipata hati hii kwani msimamizi wake ni Ofisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Ofisi ya Rais".

Alisema Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman pia alisema hajawahi kuiona sheria hiyo.
Utata wa saini
Kuhusu utata wa saini za Nyerere na Msekwa kwenye hati hizo, Nahodha alisema yeye siyo mtaalamu wa maandishi kubaini kuwa hati hizo na saini zake ni halali au la.
Hata hivyo, alisema Msekwa alikiri kwenye kamati hiyo kuwa saini iliyopo kwenye hati ya makubaliano ya Muungano ni yake.

Utata wa saini za Msekwa uliibuliwa na baadhi ya wajumbe ambao walihoji tofauti baina saini iliyopo kwenye sheria hati ya muungano na saini zake katika nyaraka nyingine rasmi.
Wajumbe waliombana Msekwa wakiongozwa na Godbless Lema, pia walitilia shaka matumizi ya kompyuta katika sheria hizo zilizoandikwa mwaka 1964.
"Mwaka 1964 hakukuwa na kompyuta lakini hapa tunaona sheria zimeandikwa kwa kompyuta na hata sehemu ya saini ya Msekwa na Nyerere kuna herufi zimeandikwa kwa kompyuta," alinukuliwa Lema.
Katika maelezo yake Msekwa licha ya kukiri upungufu, aliwakumbusha wajumbe kuwa siku ya kusainiwa hati hizo, picha zilipigwa na zipo hadi sasa.
Kamati zapiga kura

Jana jioni kamati zilianza kupigia kura sura ya kwanza, na Mwenyekiti wa Kamati Namba 5, Hamad Rashid Mohamed alithibitisha kuwa asilimia 90 ya wajumbe wa kamati yake walipiga kura za wazi kupitisha ibara za sura ya kwanza.
Alisema ibara ya 1(1) ilikubaliwa na wajumbe wa kamati hiyo kwa kupata theluthi mbili ya kura kwa upande zote, lakini katika ibara hiyo sehemu ya pili (2), haikuungwa mkono baada ya kukosa theluthi mbili kwa pande zote za Muungano.

Kifungu hicho kinatamka kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.

Hamad alisema ibara nyingine zilizokosa theluthi mbili kwa Tanzania Bara na Zanzibar ni pamoja na ibara ya 2, 5 na saba. Katika Sura ya kwanza yenye ibara tisa ni tano tu zilizokubaliwa na kamati yake.

Hamad alisema wanatarajia kukutana na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta kuangalia jinsi ya kutengua kanuni ili kuongeza muda wa majadiliano kwenye ibara ya sita ambayo wameanza kuifanyia kazi jana jioni.
Hali katika kamati nyingine tatu, ambazo wenyeviti wake hawajatoa taarifa rasmi bado, mabadiliko ya kifungu hicho yamekosa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe Zanzibar, huku katika kamati moja kifungu hicho kikikosa kuungwa mkono na theluthi mbili ya pande mbili za Muungano.
0 comments

Kesi ya Ponda ngoma nzito

Kesi ya Ponda ngoma nzito

ponda_249da.jpg

Kesi inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, imeendelea kusota mahakamani hadi hapo jalada lake litakaporudishwa toka Mahakama Kuu.Akiahirisha kesi hiyo jana hadi Aprili 16, Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro, Marry Moyo, aliitaka Idara ya Upelelezi kufuatilia jalada la mtuhumiwa huyo Mahakama Kuu ili kesi ianze kusikilizwa.

Akionekana mwenye afya njema, Sheikh Ponda anayetetewa na wakili Batheromeo Tharimo, alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi licha ya kutokuwepo umati mkubwa wa wafuasi wake.

Mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo, wakili Tharimo alidai kuwa amewasiliana na wakili mwenzake, Juma Nassoro, ambaye naye anamtetea Sheikh Ponda, na kwamba kuna ombi waliliwasilisha Mahakama Kuu la kutaka shauri hilo kutoendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro. 


Katika ufafanuzi wake juu ya madai hayo, wakili Tharimo alisema kuwa ombi hilo linatokana na rufaa namba 98 ya mwaka 2013 waliyoikata Mahakama Kuu inayohusu Mahakama ya Kisutu kwa shitaka la kwanza la kutotii amri halali ya Mahakama ya Kisutu linalomkabili mshitakiwa huyo mahakamani hapo.

Wakili huyo ambaye alidai kuwa uendeshaji wa kesi hiyo hautaendelea hadi uamuzi wa rufaa waliyoikata Mahakama Kuu utakapotolewa, aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutaja kesi hiyo.

Hata hivyo, uliibuka ubishani wa kisheria kati ya wakili Tharimo na wakili wa serikali, Sunday Hiela aliyedai kuna kumbukumbu zinaonyesha kuwa Sheikh Ponda alimkana wakili Tharimo.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger