Wilaya 31 za Tanzania zakutwa na madini ikiwamo wilaya ya Handeni na Kilindi mkoaani Tanga
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Utafiti huo ulifanywa kwa kutumia vifaa vya kisasa kama ndege kwa ajili ya kupima ramani kwenye maeneo yenye madini.
Hayo yalibainishwa katika kongamano la uzinduzi wa taarifa za
utafiti wa Fizikia ya Miamba (Jiofizikia) uliofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam,
jana.
“Tunachokifanya hapa, ni kujua kiasi gani cha madini yaliyopo
nchini. Huu ni mradi mkubwa sana, tulitumia teknolojia ya kisasa kwa
kutumia ndege angani, tofauti na tafiti zilizokuwa zinafanywa miaka ya
70,” alisema Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
wakati akizindua taarifa hizo.
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, mradi huo ni wa mara ya kwanza
kutumia vyombo vya kisasa kujua madini yaliyopo chini ya ardhi ya
Tanzania, ulihusisha wilaya 31 ambazo ziligundulika kuwa na madini ya
aina mbalimbali.
Alitaja wilaya hizo kuwa ni pamoja na Dodoma, Bahi, Chamwino,
Kongwa, Mpwapwa, Kondoa, Manyoni, Ikungi, Singida, Mkalama, Iramba,
Igunga, Kiteto, Hanang na Babati.
Nyingine ni Simanjiro, Mbulu, Arumeru, Monduli, Moshi,
Handeni.Kilindi, Korogwe, Chemba, Mvomero, Kilosa, Gairo, Bagamoyo,
Chunya, Mbozi na Mbarali.
Alisema ramani hizo zilizinduliwa jana zilikuwa zinaonyesha maeneo
yenye madini nchini na ramani hizo si kwa ajili ya rasilimali hizo bali
pia huweza kutumika kwa matumizi mengine kama vile uchorongaji wa ardhi
na upangaji miji.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa GST, Profesa Abdulkarim Mruma,
alisema, takribani Dola za Marekani bilioni 11, zilitumika katika mradi
huo wa utafiti na kutaja changamoto ni teknolojia.
Profesa Mruma, alisema baada ya kumaliza katika wilaya hizo 31,
masuala ya kifedha yakikaa sawa, wanatarajia kuendelea kufanya utafiti
na kupima ramani za jinsi hiyo katika wilaya zingine za Nachingwea,
Mpanda, Sumbawanga na Songea na kwamba maeneo ambayo yamegundulika kuwa
na madini, yatatangazwa kwa wananchi kwa utaratibu maalumu uliowekwa na
serikali na Watanzania wanapaswa kuwa na leseni kwa ajili ya kunufaika
na rasilimali hizo.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment