MANJI AWAOMBA WADHAMINI WA KLABU KUANGALIA UPYA MKATABA WA AZAM TV

MANJI AWAOMBA WADHAMINI WA KLABU KUANGALIA UPYA MKATABA WA AZAM TV


Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amewaomba wadhamini wa klabu hiyo, kuangalia upya mkataba wa Azam TV, kwani kwake yeye binafsi anauona hauna manufaa kwa klabu yao ambayo inaingiza zaidi ya mil 300 katika mchezo mmoja akitolea mfano mchezo kati yao na Watani zao Simba.

Baada ya kusema hayo, Manji aliwataka wanachama kutoa maoni yao juu ya suala hilo, ambapo Patric Mandewa kutoka Mwembeyanga aliunga mkono hoja ya Manji na kusema kuwa, hawaoni faida ya kuchukua mil 100 kutoka Azam TV wakati wao ni klabu kubwa ambayo inauwezo wa kujisimamia na katika mechi moja ikapata zaidi ya fedha hizo.

Mbali na hayo, wanachama wakiongozwa na Tuni Bakar 'Mama Tuni' walilazimika kumpigia magoti Manji ili kumuomba kupangua kauli yake ya kutotaka kugombea tena, nafasi ya Uenyekiti ambayo bado anaishikilia mpaka sasa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Loyd Nchunga kujiudhuru.

Licha ya wanachama hao, kumtaka Manji kupangua kauli hiyo, Manji aliendelea na msimamo huohuo huku akiwataka wanachama kuachana na hoja hiyo kwani haina mashiko katika maendeleo ya Yanga kwa kuwa uongozi ni demokrasia, na kujikuta akiharibu hali ya hewa baada ya kauli hiyo na wanachama kuanza kuondoka ndani ya ukumbi huo.

Baada ya wanachama kuondoka, Mc wa Mkutano huo, Bakiri Makere aliwataka wanachama kutulia huku akisema 'Yanga Oyeee' na kujikuta akikosa wa kumjibu kama ilivyokuwa awali kabla ya Manji kujibu kwa msisitizo kuwa hatagombea tena kiti hicho.
Uongozi wakili kikosi kuwa dhaifu....

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umekiri kikosi chao kuwa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja huku wakidai hiyo ndiyo sababu ya timu yao kutofanya vema katika michezo mbalimbali ambayo imechezwa hivi karibuni licha ya kuongoza ligi.

Hayo yalisema na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ambaye aliwaweka wazi wanachama wa klabu hiyo, sababu za kutimua benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Ernie Brandts na msaidzi wake Fred Felix 'Minziro'.

Sanga alisema, walifikia hatua hiyo, baada ya kuona benchi la ufundi linashindwa kufanya kazi na kujikuta wakipanga vikosi kwa mazoeza bila ya kutazama uwezo wa mchezaji mwenyewe na kuangalia majina.

"Timu ina wachezaji wazuri lakini ni mmoja mmoja, timu haichezi kitimu ni ngumu kufanya vizuri, na ndio maana tukachukua hatua hiyo, na huu ni mwanzo kwani hata wachezaji wenye utovu wa nidhamu atautaangalia jina la mtu wala nini tunamwajibisha tu,"alisema Sanga na kuongeza kuwa, hata wachezaji wanaocheza mchangani watawashughulikia.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger