Viongozi
hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja
kuelekea nyumbani. Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa
akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo
ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba
wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said
Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia alifariki dunia Januari 22, 2014
katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya
Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo
nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
PICHA NA IKULU
|
Post a Comment