SIMBA SC KAMILI GADO ZENJI, LOGARUSIC RAHA TU IVO NA OMWANWA NDANI YA NYUMBA, YANGA WAANDAE KAPU JUMAMOSI TAIFA

SIMBA SC KAMILI GADO ZENJI, LOGARUSIC RAHA TU IVO NA OMWANWA NDANI YA NYUMBA, YANGA WAANDAE KAPU JUMAMOSI TAIFA

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KIKOSI cha Simba SC kimekamilika kambini eneo la Chukwani, Zanzibar kufuatia wachezaji wapya kutoka Gor Mahia ya Kenya, kipa Ivon Philip Mapunda na beki Donald Mosoti Omwanwa kujiunga na wenzao jana visiwani humo, tayari kwa mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na wachezaji hao wawili waliosajiliwa wiki iliyopita, wachezaji wengine wapya waliosajiliwa dirisha dogo, kiungo Awadh Juma na mshambuliaji Ally Badru nao pia wameingia kambini jana.
Beki 'Adui'; Donald Mosoti Omwanwa tayari yuko kambini na Simba SC Zanzibar

Badru na Awadh walikuwa na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, michuano iliyomalizika Alhamisi iliyopita nchini Kenya.
Kocha mpya wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic ameingia kambini na wachezaji wote waliosajiliwa kuandaa kikosi cha kuiadabisha Yanga Jumamosi Uwanja wa Taifa.    
Furaha zaidi kwake ni kwamba, wachezaji alioomba mwenyewe wasajiliwe Ivo na Omwanwa wamewasili mapema na sasa Jumamosi atakuwa na jeshi kamili la kuanzisha zama zake mpya Simba SC.
Simba SC ambayo mara ya mwisho ilitoa sare ya 3-3 na Yanga ikitoka nyuma kwa mabao 3-0 hadi mapumziko, inaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuoni na inatarajiwa kurejea Dar es Salaam siku moja kabla ya mechi ya Mtani Jembe.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger