"KAMA SI KANUMBA YANGENIKUTA MAZITO.." LULU AFUNGUKA

"KAMA SI KANUMBA YANGENIKUTA MAZITO.." LULU AFUNGUKA

SURA ya mauzo katika sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ 

ametoa ya moyoni kuwa kama siyo kuwekwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya Segerea, Dar basi yangemkuta mazito.


Lulu alikaa Gereza la Segerea kwa takribani miezi kumi baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ 
aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.

Nyota huyo wa Filamu ya Foolish Age alifunguka mambo ya kushangaza hivi 
karibuni juu ya tukio hilo kupitia Kipindi cha Take-One, kinachorushwa  na 
Clouds TV.
 TATIZO FOOLISH AGE
Lulu alikuwa akizungumzia filamu yake hiyo ya Foolish Age ambapo 
alisema sinema hiyo inawasihi wasichana ambao wanapitia kipindi cha balehe 
ambacho ni hatari sana kwao.

“Kwa kweli kipindi cha foolish age ni cha hatari sana, nilicheza filamu hiyo
 ili kuwaasa wasichana wenzangu.
“Asikwambie mtu, mimi mwenyewe nilikokuwa nikielekea si kuzuri kabisa.

 KAMA SIYO KANUMBA
“Ukweli ni kwamba kama siyo matatizo (kifo cha Kanumba) nikaenda 
mahabusu sijui ingekuwaje sasa hivi. Kukaa jela kulinisaidia kusitisha kasi ya 
tabia yangu, nikatoka nikiwa mpya.
“Yangenikuta mazito zaidi maana kipindi kile ilikuwa hatari tupu,”
 alisema Lulu ambaye ni mrembo wa haja.
 Staa huyo aliongeza kuwa kipindi hicho kilikuwa cha hatari na hakitamani 
kijirudie hata kidogo katika maisha yake.
Alisema kwamba si ajabu inawezekana kipindi hicho ndicho kilisababisha 
matatizo yote yaliyomkuta. Alisema alikuwa akielekea kubaya.
 HATAKI KIJIRUDIE
“Ni kipindi ambacho siwezi kukuhitaji tena katika maisha yangu si kizuri 
na kinatisha maana kuna wakati nilikuwa sisikii la mtu yeyote hata mama 
yangu mzazi,” alisema Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu haonekani
 akirandaranda mjini kama zamani.

Kabla ya utulivu huo alioupata nyuma ya nondo, Lulu alikuwa hakauki 
kwenye kumbi za usiku za starehe huku akilewa tilalila na kuyaweka 
maisha yake hatarini endapo angefanyiwa kitu mbaya.

 Lulu alihusishwa na kifo cha Kanumba kwa kuwa siku ya tukio alidaiwa kuwa 
naye eneo la tukio ambapo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana 
akisubiri kesi ya kuua bila kukusudia.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger