ZIUNGENI MKONO TAASISI ZINAZOPAMBANA NA UKATILI NA UNYANYASAJI WA WANAWAKE NA WATOTO-TUNU PINDA.
![]() |
MKE WA WAZIRI MKUU WA TANZANIA MAMA TUNU PINDA AKIZUNDUA KAMPENI YA TANGA TUNAWEZA LEO ILIYORATIBIWA NA ASASI YA TREE HOPE. |
Na Paskal Mbunga,Tanga.
MKOA wa
Tanga umehimizwa kuziunga mkono taasisi zinazopambana dhidi ya ukatili na
unyanyasi kwa wanawake na watoto ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu
zinalindwa.
Akizindua
rasmi
leo kampeni ya “Tunaweza Mkoa wa Tanga” inayoerndeshwa na asasi ya Tree
of Hope ya jijini hapa, Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda alisema suala la
ukatili wa kijinsia katika
jamii yetu linaendelea kushika kasi na kuleta madhara mengi yakiwemo
ulemavu
mwilini, msongo wa mawazo, kuvunjia kwa ndoa ama kusababisha wanandoa
kuathiriwa na magonjwa hatari, ukiwemo UKIMWI, na wakati mwingine vifo.
Mama
Pinda
alisema kwamba Mkoa wa Tanga umefikisha asilia 15.7 kwa ukatili wa
kimwili
(physical violence) na asilimia 11.3 ya matukio ya ukatili wa kingono
(sexual violence). Hii ni kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa
mwaka 2010 (Tanzania Demographic & Health Survey),
Mke wa
Waziri Mkuu ambaye alionekana kutishwa na takwimu hizo, aliutaka uongozi wa
Mkoa wa Tanga kuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha kuwa haki za binadamu
zinalindwa huku akionya kwamba hali hiyo sio ya kufumbiwa macho.
Alisema
ili kupambana na hali hiyo, Serikali ya Tanzania ilitunga sera ya Jinsia ya
mwaka 2000 ikiandaa Mkakati wa miaka 15 wa kuondoa ukatili kwa wanawake na watoto
katika jitihada ya kukabiiliana na changamoto hizo.
Mama Pinda
alikemea tabia potofu zilizozoeleka miongoni mwa wanawake kwamba kupigwa na
mume ni jambo la kawaida na linalokubalika kwa baadhi ya makosa ambayo mwanamke
anapomkosea mumewe ni lazima aadhibiwe.
Alitaja
mazoea hayo ni pamoja na kuafiki kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo
ataondoka bila kuaga kwa mume. Pia mume ana haki ya kumpiga mkewe endapo
atazembea kuangalia watoto. Pia tabia
nyingine ni mke kukubali kupigwa na mume kutokana na kubishana naye.
Mama Pinda
alizitaka asasi za kiraia kuungana pamoja katika mapambano dhidi ya ukatili wa
kinsia na kusisitiza kwamba kampeni ya “Tunaweza”Ni mkakati
muhimu katika kutokemeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Awali,
akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa aliwataka wakinamama kuiunga mkono kampeni
hiyo kwa kujishughulisha na miradi ya uzalishaji mali ambayo kwayo itawaweka
huru pasi na utegemezi mkubwa kutoka kwa wanaume.
Aliwataka akinamama kuzitumia
taasisi ya kifedha kwa ajili ya kujijengea mitaji ya kufanya biashara.
Kwa
upande wake,Mratibu wa Asasi ya Tree of Hope FortunataManyeresa
aliitaka jamii kuwa mstari kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo
kuwalinda watoto na wanawake.
Alisema
asasi hiyo tayari imeshaeneza huduma zake katika wilaya zote nane za
mkoa wa Tanga lengo likiwa ni kuhamasisha wakazi wa mkoa wa Tanga kupata
mwamko wa kuweza kupambana na tatizo hilo ambalo lilojengeka kwa
misingi ya tamaduni za kikabili
Post a Comment