STEWART HALL APATA KAZI SUNDERLAND

STEWART HALL APATA KAZI SUNDERLAND

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA Muingereza, Stewart Hall atakuwa Kocha Mkuu wa akademi ya Symbion Power inayoanzishwa nchini kwa ushirikiano wa klabu ya Sunderland AFC ya England na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.
Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Tanzania, Peter Gathercole, amesema leo kwamba akademi hiyo itakuwa na vituo Kidongo Chekundu (Sports Park) na Elite Football Academy, Dar es Salaam.
Stewart Hall enzi zake Azam FC

Hall, mwenye leseni ya UEFA ya ukocha na Mkufunzi wa shirikisho hilo, amepewa kazi hiyo baada ya mafanikio yake akiwa na klabu ya Ligi Kuu, Azam FC na timu ya taifa ya Zanzibar na Birmingham City alipokuwa Mkurugenzi wa akademi.  
Kabla ya hapo, Hall alikuwa kocha wa timu za taifa za Saint Vincent na Grenadines, pamoja na Pune FC ya India. 
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Hall alisema, “Mradi huu hakika utasaidia kuinua soka ya vijana kwa viwango vyote, timu za taifa na klabu. Vijana wadogo watafundishwa ufundi, mbinu, kujengewa uimara wa kimchezo na maarifa ya soka ya kisasa,”alisema.
Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC, Margaret Byrne, amesema: “Tunafurahi mradi wa akademi unaendelea vizuri. Kuteuliwa kwa  Stewart ni hatua ya kufurahisha na tunatarajia kila mmoja kufanya kazi kwa bidii ili kuvuna matunda baadaye.”
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, alitemebelea akademi ya Sunderland akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete Juni mwaka huu ambako walifikia makubaliano na Sunderland AFC na Symbion Power Tanzania juu ya mradi huu.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger