Naibu Meya na diwani wa kata ya Kiboriloni, Vicent Rimoy afariki Dunia

Naibu Meya na diwani wa kata ya Kiboriloni, Vicent Rimoy afariki Dunia

BREAKING NEWS:NAIBU MEYA MANISPAA YA MOSHI AMEFARIKI DUNIA....

Diwani Rimoy
Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
NAIBU Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, (Chadema), Mhe. Vincent Rimoy (pichani), ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kiboriloni(chadema) amefariki dunia Ghafla Leo, majira ya saa 11:30 asubuhi akiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kupata matibabu.


Akizungumzia kifo hicho, Meya wa Manispaa ya Moshi, na  Mstahiki Jaffari Michael, alithibitisha taarifa za kifo hicho ambapo  alisema Mhe. Rimoy alifariki wakati akikimbizwa hospitali baada ya kudondoka akiwa shambani kwake eneo la Mandaka, wilaya ya Moshi.


“Ni kweli amefariki na muda siyo mrefu jamaa zake tayari wameshakwenda  kuuhifdhi mwili wa marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti cha  hospitali ya Rufaa ya KCMC”, alisema Meya huyo ambae pia ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Moshi Mjini.

 

Rimoy ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la Damu, alikutwa na umauti huo baada ya awali kufikishwa katika Zahanati ya Jaffar ambako alipewa huduma ya kwanza na Daktari wa Zahanati hiyo
ambaye hata hivyo alishauri apelekwe katika Hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.

 

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wake ambaye hakutaka jina lake litajwe, Mhe. Rimoy aliamka asubuhi na kwenda shambani kwake baada ya kutoka safari ya Dar es Salaam juzi.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger