MWENYEKITI CCM WILAYA YA TANGA AWAAGIZA WATENDAJI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KWA UKARIBU.

MWENYEKITI CCM WILAYA YA TANGA AWAAGIZA WATENDAJI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KWA UKARIBU.

Na Amina Omari,Mzizima.
Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi Wilaya ya TangaKassim Mbuguni amewaagiza watendaji wa mitaa,vitongoji na kata kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo kwa ukaribu katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho  na kama wakishidwa waachei ngazi.

Agizo hilo alilitoa wakati wa uzinduzi wa shina la Vijana wa nguvu

kazi wa  Chama Cha Mapinduzi UVCCM kata ya  Mzizima mwishoni mwa wiki ambapo alisema kuwa haiwezekani kuwa na watendaji ambao hawasimami wa kutekekeleza ilani ya chama.

Alisema kuwa ifike mahali ni lazima tuwe na watendaji ambao

tunaendanao kwenye maamuzi yetu sio kuwa na ambao wanatupinga na kurudisha nyuma maendeleo pamoja na kasi katika kuwasogezea huduma wananchi.

“Salamu nazitoa kwa watendaji ambao watashindwa kusimamia na

kutekeleza miradi wajitoe wenyewe,Ni aibu kwa mtendaji wa mtaa
kushindwa kusimamia mradi mdogo wa darasa moja la shule halafu
unajiita mtendaji hutufai katika mbio zetu za kuleta maendeleo jitoe
mapema kabla hatujakutoa kwa nguvu”Mbuguni.

Pia aliwashauri watendaji hao kuacha kukaa ofisi pekee na kusubiri

taarifa kwenye makaratasi bali wahakikishe wanashuka hadi katika ngazi za chini za wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi wa haraka .

Aliongeza kuwa sifa ya kiongozi bora aliyechaguliwa na wananchi ni
kuhakikisha anawasikiliza na kuwatatulia kero zao wanazokabilianazo waliomchangua na sio kusubi maamuzi kutoka ngazi za juu pekee.

“Nawapa taarifa nitaanza kupita kuanzia ngazi za mitaa,kata na

vitongoji katika Jiji hili na  kukagua maendeleo na changamoto
zilizopo Na jinsi zilivyotatuliwa na viongozi wa serikali nitakapo
baini mapungufu hatabaki mtu nitamtoa kwa aibu “alisisitiza Mbuguni.


Katika Hatua nyingine alimuagiza Diwani wa Kata hiyo Daniel Mgaza
  kuhakikisha na maliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji na umeme katika kata hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ili wananchi hao wasiendelea kuteseka na kero hizo.

Alisema kuwa diwani ni ndio msimamiaji sera na ndiuo aetetea wananchi
katika kata yake hivyo tatizo la maji na umeme kuikabili kata hiyo tena ipo mjini ni jambo la aibu hivyo ni vemna ahakikishea ameimaliza mapema kero hiyo.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger