Dr. Slaa Awaonya CCM na Kikwete Kutokufanya Usanii Na Maisha Ya Watanzania
Dr. Slaa amependezwa kuona jinsi wanafunzi na wanajeshi wanavyoshirikishwa katika utafiti kwa manufaa ya nchi. Dr. Slaa alijionea mashine ya ndogo ya aina yake inayotumia takataka na hata majani kutengeneza umeme pamoja na gesi ya hydrogen kwa wakati mmoja, mtambo uliogunduliwa kwa ushirikiano kati ya chuo kikuu cha Indiana na Jeshi la Marekani.
Bahati mbaya wanafunzi kama hawa nchini kwetu serikali imewanyima nafasi ya kukuza vipaji vyao na kutusaidia kwenye maswala ya utafiti. Wanajeshi wetu waadilifu, wachapakazi na wazalendo wamekatishwa tamaa. Gari la nyumbu walilotengeneza linaoza na mradi mzima umekufa. Wastaafu wametelekezwa hadi malipo yao wanadhulumiwa na serikali dhalimu ya CCM. Hiyo ndiyo CCM
Kwa miaka zaidi ya 50, serikali ya CCM imekuwa ikitoa ahadi za kumaliza tatizo la umeme. Mpaka sasa, CCM bado wanaendelea na ahadi zao kana kwamba watanzania bado wamelala. Ni swala la fedheha na aibu kubwa kwa nchi kama Tanzania kuzunguka kuomba misaada wakati tunacho kila tunachohitaji kujitengenezea umeme wa kutosha alisema Dr. Slaa
Tanesco ambayo ingekuwa inatutengenezea umeme wa kutosha kwa matumizi yetu na kuuza nje ya nchi umeme wa ziada, imegeuka kuwa shamba la bibi na kichaka cha mafisadi. Wizara nayo imekuwa makao makuu ya matusi kwa wawekezaji na watanzania. Waziri muhongo badala ya kutafuta suluhisho ya matatizo yeye amekuwa mtambo wa matusi. Anawaambia watanzania wakawekeze kwenye juice na matunda. Hii ndio maana tunasema kwamba CCM ni janga la mtanzania
Tunachotaka kujua ni Uhusiano wa Symbion na serikali ya CCM. Tunataka kujua hii kampuni ya Symbion inamilikiwa na nani . Kwa sababu ni hii Symbion ndiyo ilitokana na Dowans ambayo ilizaliwa na Richmond. Makampuni ambayo yanatafuna kodi zetu hadi wa leo. Wanatudanganya watawashtaki mafisadi wa Tanesco, tunawaomba waanze na mafisadi papa wa EPA na Richmond
Rais Kikwete na CCM wamekuwa janga. Leo Kikwete anaagiza shule zote za kata ziwekewe umeme. Umeme gani wanaozungumzia na utatoka wapi wakati wameshindwa katika kipindi cha miaka zaidi ya hamsini. Watanzania wamechoshwa na usanii. CCM wamebaki kugawana vyeo kindugu na kirafiki. Hawana uchungu na nchi, wanachojali ni kiasi gani wataweza kuiba. Inabidi watanzania wajitayarishe kuin’goa CCM madarakani kupitia sanduku la kura alisema Dr. Slaa.
Mwanafunzi wa Kitanzania katika chuo cha Indiana akimpokea Dr. Slaa
Kutoka Kushoto, Mwanafunzi wa Kitanzania, Dr. Slaa, mwanajeshi mtafiti pamoja na Mwenzie ambaye ndiye kiongozi wa utafiti
Dr.
Slaa akikagua mtambo wa utafiti uliogunduliwa na Wanafunzi na walimu
katika chuo cha Utafiti wa Indiana. Mtambo ni wa kutengenezea gesi ya
hydrogen pamoja na umeme mbadala (renewable energy) unaopatikana
kutokana na takataka
Meya pamoja na mkuu wa polisi nao walikuja kumuona Dr. Slaa na kumkaribisha kwenye jiji lao
Dr.
Slaa baadae jioni alikutana na wakurugenzi wa mashirika makubwa ya
nishati (renewable energy) nchini marekani ambao wako tayari kufanya
kazi na CHADEMA kuiletea Tanzania umeme wa bei nafuu. Baadhi ya hawa
wawekezaji wamewahi kuja Tanzania lakini Tanesco kama kawaida yao
wakawakwamisha. Chadema inajipanga kuwaletea watanzania unafuu
wanaoulilia
Viongozi wa chuo kwenye picha ya pamoja na Dr. Slaa
Post a Comment