WIZARA YA UCHUKZI WAKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA CHINA
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire
(kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Wizara na
ujumbe kutoka Kiwanja cha ndege cha Guang Dong kutoka nchini China,
wakati ulipotembelea Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Ujumbe umeonyesha
nia kuwekeza katika Viwanja vya Ndege vya Tanzania. (Habari Picha
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire
(kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Guang Dong cha
nchini China, Bw. Wen Wenxing wakati ujumbe huo ulipokutana na uongozi
wa Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen
Wenxing (kushoto), akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa
Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi baada ya
ugeni huo kukutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi.
Post a Comment