LEWANDOWSKI NI KAMA TAYARI AMEKWISHATUA BAYERN, MWENYEWE ASEMA ANAHAMIA BAVARIA JANUARI
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund,
Robert Lewandowski hatimaye amethibitisha atasaini kama mchezaji huru
kujiunga na wapinzani, Bayern Munich ifikapo Januari na kuhamia Bavaria
Mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.
Anaondoka: Robert Lewandowski amethibitisha kuondoka Borussia Dortmund kuhamia Bayern Munich mwakani
Baada ya tetesi kadhaa miezi ya majira
ya joto, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka
25 ataungana na kabi ya Pep Guardiola, Lewandowski ameacha Mkataba wake
umalizike na ataruhusiwa kusaini Mkataba wa awali kujifunga Allianz
Arena mwaka 2014.
Kwa mara ya kwanza tangu azuiliwe na
kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp aliyegoma kuwauzia silaha yake wapinzani
wake wa Bundesliga, Lewandowski amesema atajiunga na Munich kama
mchezaji huru.
Akijibu swali kwamba atahamia Signal
Iduna Park Januari, Lewandowski alisema: "Ndiyo, kwa sababu baadaye
nitasaini Mkataba rasmi,"
Njia iko wazi kwa Lewandowski kujiunga
na mabingwa hao wa Ulaya baada ya kocha wa zamani wa Barcelona,
Guardiola kumruhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Mario Gomez
kutimkia Fiorentina, na kutoa nafasi kwa mshambuliaji mwingine.
Mtambo wa mabao: Lewandowski amefunga mabao manne Dortmund katika mechi sita za Bundesliga msimu huu
Dole: Kocha wa Bayern, Pep Guardiola amemruhusu Mario Gomez kuondoka, na kutoa nafasi ya Lewandowski kutua
Kuondoka kwa Lewandowski kutaacha pigo
katika safu ya ushambuliaji ya Dortmund – ambako amefunga mabao 58
katika mechi 103 tangu ajiunge nayo mwaka 2010 kutoka Lech Poznan ya
Poland.
Mwaka jana alifunga mabao 36 katika
mashindano yote pamoja na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza
kufunga mabao manne katika Nusu Fainali moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
timu yake ikishinda 4-1 dhidi ya Real Madrid, kabla ya kufungwa na
Bayern 2-1 katika Fainali, Uwanja wa Wembley, Mei mwaka huu.
Licha ya Munich kununua zaidi wachezaji
bora na wa bei kubwa, bado timu zote zimefungana kileleni mwa Bundesliga
baada ya mechi sita, kila timu ikiwa na pointi 16 na kutofautiana kwa
wastani wa mabao tu ya kufunga na kufungwa
Post a Comment