RC TANGA AONGOZA MAPOKEZI YA COASTAL UNION "MABINGWA WA KOMBE LA UHAI"

RC TANGA AONGOZA MAPOKEZI YA COASTAL UNION "MABINGWA WA KOMBE LA UHAI"

Na Oscar Assenga, Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa jana aliwaongoza wakazi wa mkoa katika mapokezi ya kuipokea timu ya Vijana ya Coastal Union ambao ni mabingwa wapya wa Mashindano ya Kombe Uhai Cup baada ya kuifunga Yanga kwenye mechi ya Fainali.

Maandalizi ya mapokezi hayo yalianza majira ya saa nane mchana kwa shamrashamra za aina yake huku barabara iliyokua ikielekea kwenye uwanja wa Mkwakwani ilifurika umati mkubwa wa mashabiki wake.

Akizungumza baada ya kupokea kombe hilo, Gallawa ushindi huo ni ishara tosha kuwa historia ya soka mkoa wa Tanga inajirudia kama ilivyokuwa hapo awali hivyo vijana waendelee kujipanga ili kuendelea kupata mafanikio zaidi.

   “Mimi nina furaha kwa sababu mmeijengea heshima Tanga kwa maana ya mkoa mzima na mmenisaidia na kuendelea kufundisha kuwa hakuna kisichowezekana kazi mliyofanya ni mzuri na muendelee kupambana ili muweza kupata mafanikio zaidi “Alisema Gallawa.

Awali akizungumza katika mapokezi hayo, Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union, Hemed Aurora aliwapongeza wachezaji hao kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo na kueleza ushindi huo umewapa heshima kubwa.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger