UHAMIAJI TANGA WAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VIFAA VYA BAHARINI
Na Raisa Said,Tanga
IDARA ya Uhamiaji mkoani Tanga inakabiliwa na changamoto ya Ukosefu wa vifaa vya baharini boti na meli kwa ajili ya doria za baharini dhidi ya wahamaaji haramu wanaongia nchini kwa njia za mwambao wa Pwani.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Sixtus Nyaki wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu hali ya wimbi la uhamiaji haramu katika Mkoa huu kwa sasa, ambapo alisema kwa sasa wanalazimika kutumia boti la jeshi la polisi mkoani.
“ Tunatumia boti moja la polisi kwa ajili ya doria za mara kwa mara za baharini ,kitu ambacho wakati
mwingine tunashindwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kutoka na
boti hiyo kutumika kwa doria nyingine na Jeshi la Polisi”alisema Nyaki.
Nyaki
alisema ukubwa wa mipaka ya baharini hadi nchi kavu ni mikubwa hivyo
kusababisha kushindwa kuithibiti kwa pamoja hali inayosababisha
wahamiaji haramu wengi kuvuka na kuingia nchini kwanjia za panya.
Afisa huyo
alisema ushiriki wa wananchi katika biashara ya kusafirisha wahamiaji
haramu imekuwa ni chanzo cha tatizo hilo kuwa kubwa kwani wengi wao
wanategemea kuishi kwa kusafirisha wahamiaji hao na kuchangia ongezeko
la wahamiaji hao.
Hata hivyo aliongelea juu ya kiasi cha wahamiaji haramu waliokamatwa katika kipindi cha Octoba hadi sasa kuwa ni kiasi cha wahamjia 68 wamekamatwa sehemu mbalimbali za mkoa huu.
Aliwataja wahamijai hao waliokamatwa kuwa wengi ni kutoka katika nchi ya Ethiopia na wengine kutoka nchi mbalimbali duniani hapa na wengine wakiishi nchini kinyume cha sharia.
Wahamiajia hao na idadai yao ni Waethiopia 48,Wakenya 6,Waganda 5,Wajerumani 3,Wanaijeria 2,Mreno 1,Msomali 1,naraia wa Peru 1.
Post a Comment