Kampuni ya madini ya Canaco yathibitisha wingi wa dhahabu wilayani Handeni, mkoani Tanga

Kampuni ya madini ya Canaco yathibitisha wingi wa dhahabu wilayani Handeni, mkoani Tanga

Na Amina Omari, Handeni
WILAYA ya Handeni ni kati ya maeneo yaliyobarikiwa kuwa na rasilimali nyingi, yakiwamo madini aina ya dhahabu nchini Tanzania, huku kwa kikubwa  yakipatikana katika milima ya Magambazi, Km 30 kutoka Handeni mjini.
Msimamizi Mkuu wa Kampuni ya utafiti wa madini ya Canaco Tanzania Ltd, Bavon Mwaluko akiwaonyesha waandishi wa habari sampuli za udongo zilizofanyiwa utafiti na kampuni yake kwenye mlima wa Magambazi Wilayani Handeni, Mkoani Tanga na matokeo kuonyesha kuwa eneo hilo lina madini aina ya dhahabu yenye ubora mzuri.
Kuwapo kwa rasilimali hiyo kumeweza kuisaidia wilaya hiyo kimapato pamoja na wananchi kwa nia ya kujikimu kimaisha juu ya shughuli za uchimbaji na uuzaji wa madini kwa ujumla.


Sampuli ya udingo uliotumika kufanyia utafiti na Kampuni ya utaifiti ya Canaco Tanzania Ltd wakati wa kazi ya kutafiti madini kwenye mlima wa Magambazi Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga kazi hiyo ilifanyika tangu mwaka 2007 na mwaka jana ikatoka na mtokeo yanayoonesha kuwa eneo hilo lina madini aina ya dhahabu yenye ubora na daraja zuri.



Pia kuwepo kwa madini hayo kunawavutia watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi kuja kutafuta madini hayo.
Mfanyakazi wa Kampuni ya utafiti wa madini ya Canaco Tanzania Ltd, akichambua sampuli za udongo uliochimbwa katika mlima wa Magambazi ambao utafiti umeonyesha kuwa yapo madini yenye ubora na daraja zuri katika soko.


Awali eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na wachimbaji wadogo waliokuwa wanatumia zana duni za kuchimba pamoja na kukabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya vifaa vya uchimbaji.
Jambo hilo limewafanya wakati wote waonekane ni masikini na wanaopata wasiwasi dhidi ya uharibifu wa mazingira sanjari na kupata mali kidogo tofauti na matarajio ya kazi yao.
Hatua hiyo ilisababisha serikali ya Wilaya ya Handeni kuwakaribisha wawekezaji wageni ambao kwa kutumia teknolojia ya kisasa wataweza kuchimba kwa ufanisi na wakati huo huo kulipa kodi itakayofanikisha kuboresha maisha ya wananchi wote.
Kampuni hiyo si nyingine, ila ni CANACO. Hawa ni moja ya wadau wa madini waliopewa fursa hiyo ya kufanya tafiti tafiti za uwepo wa dhahabu katika eneo hilo.
Meneja Utafiti wa kampuni hiyo, Bavon Mwaluko anasema kuwa waliingia katika eneo hilo mwaka 2007 kwa ajili ya kuendesha shughuli za utafiti wa madini yaliyoko kama hatua za awali kabla ya kuanza kazi ya ujenzi wa mashine kwa ajili ya uchimbaji.

Walipoingia walikubaliana na wenyeji waliokuwa wakimiliki maeneo hayo ambao walikuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji mdogo  na walitumia fedha nyingi kuwalipa fidia ili wafanye shughuli hiyo.
Tafiti walizokuwa wanazifanya ni pamoja na kujua aina ya miamba iliyobeba dhahabu kwenye eneo hilo imeelekea upande gani pamoja na tabia za kijiolojia za mimba hiyo bila kusahau thamani ya dhahabu itakayozalishwa.
“Kabla ya kuanza zoezi la uchimbaj ni lazima kufanya tafiti ili kujua tabia za miamba ukizingatia mingine inaweza kuwa na milipuko au ni sehemu ya chanzo cha maji, hivyo shughuli hiyo kuwa na uharibifu wa mazingira,” alisema Mwaluko.
Mwaluko anasema mwaka 2008 waliendeleoa na utafiti pamoja na ukaguzi wa eneo la mradi ili kujua aina ya madini yaliyokuwapo ambapo mwaka 2009 hadi 2010 walianza rasmi uchimbaji katika eneo la magambazi baada ya matokeo ya awali kuonyesha kuwa kulikuwa na madini ya kutosha.
Mwaka 2012 walifanya utafiti wa mwisho ili kujua iwapo uchimbaji utaanza utaweza kudumu kwa miaka mingapi ili katika kazi hiyo kusitokee mkanganyiko wowote.
Anasema kuwa kampuni zinazofanya kazi ya utafiti wa madini nchini
zinapaswa kuweka wazi shughuli zao kwa wananchi ili waondokane na dhana ya kudaiwa kuwa wanahamisha malighafi hiyo na kuipeleka katika nchi zao.

“Si kweli kuwa kampuni za utafiti zimekuwa zikihamisha nje
madini bali kinachofanyika ni kupeleka sampuli ya udongo katika
maabara zilizoko mjini Mwanza na nje ya nchi kwa ajili ya kupata
matokeo.

“Wakati wa  kufanyika utafiti tunapopeleka sampuli ya udongo kwenye
maabara kuna mchakato mrefu  wenye uwazi ambao hupitia na kuchunguzwa na vyombo vya dola kama Mamlaka ya Mapato na Usalama wa Taifa na ikikamilika, lazima irejeshwe kwa utaratibu
ule ule,” Alisema.

Anasema ukweli ni kwamba kampuni zilizojikita hasa katika kutafiti
madini baada ya kupata kibali hulazimika kuwekeza kikamilifu, hivyo si rahisi kufanya hujuma zinazoweza kuhatarisha utendaji
kazi wao ndani na nje ya nchi.

Anasema nchini Tanzania maabara inayofanya kazi ya kutoa majibu ya
sampuli za madini ni moja na ipo jijini Mwanza, huku ikielemewa na wingi wa kazi wanazoepelekewa.
“Hii dhana ni potofu na inatokana na ukweli kuwa nchini hapa taaluma ya utafiti ni ngeni katika mambo mengi hivyo baadhi ya viongozi wanaamini hicho kinachosemwa,” alisema.
Juu ya uhusiano unaowazunguuka, Mwaluko anasema wakati wa shuguli za utafiti waliajiri vijana zaidi ya 300 kutoka katika maeneo yanayaozunguka eneo hili ili kuwanufaisha kiuchumi.
Anasema walishindwa kabisa kuchukuwa watu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuwapatia mwangaza wa kimaisha na kuingia katika mfumo mzuri katika mlolongo wao kimaisha.
Mbali na mazuri yote hayo, Mwaluko hakusita kusema kuwa kwa sasa shughuli zao hizo zimesitishwa kwanza na serikali, huku wakiamini kuwa wanatarajia kuwatumia vijana wengi pindia uchimbaji zitakapoanza.
Kipaumbele kwa vijana wa maeneo ya jirani kama vile vijiji vya Nyasa na Madebe ambapo wanatarajia uzalishaji utakapoanza, vijana 1000 watapata ajira ya kudumu kwenye mgodi.
Katika kusaidia miradi ya kijamii wameweza kukarabati  shule ya msingi Nyasa kwa kujenga majengo bora pamoja na kuweka thamani na kununua vitabu vya kiada kwa matumizi ya wanafunzi shuleni hapo pia kuwajengea kisima kwa ajili ya kuuzamaji ili shule iweza kupata fedha kwa matumizi yake madogo madogo.
Nae Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyasa Fabian Msofe anasema kuwa  kabla ya kampuni ya CANACO haijafika kwenye eneo hilo shule hiyo ilikuwa kwenye mazingira magumu sana  kwani kulikuwa na madarasa 3 tu ambaya nayo hayakuwa katika hali nzuri na hakukuwa na ofisi ya walimu wala mwalimu Mkuu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyasa Shaban Ali, anasema kuwa tangu kampuni hiyo iingine kwenye eneo lao wameweza kuwafanyia mambo mengi ikiwamo ujenzi wa visima virefu viwili pamoja na kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa kijiji hicho.
“Kwakweli tulikuwa tumesahaulika kwani huku Nyasa ni mbali kutoka na ubovu wa barabara lakini walipofika hawa wawekezaji wameweza kutusaidia tatizo la maji ila shida ipo kwenye zahanati kwani hakuna kwa sasa,” alisema.
Nae Mwanaid Ali anasema kuwa wanalazimika kwenda umbali wa zaidi ya Km 35 kupata huduma za afya kwenye hospitali ya Wilaya ya Handeni lakini kwa uwepo wa kampuni hii umeaidia kutupa usafiri pindi tunapo hitaji kupeleka mgonja hospitali.
“Kina mama wengi waliweza kupoteza maisha  hapo awali kutoka na ukosefu wa huduma ya afya karibu na kijiji kwani usafiri tuliokuwa tunautegemea ni pikipiki au umgonjwa akokotwe kwenye baiskeli na wanaume likiwa jambo la hatari,” alisema.
Hata hivyo Ali ameongeza kuwa chagamoto inayowakabili kwasasa ni wachimbaji wadogo wamekuwa ni kikwazo kwani kwa sasa eneo hilo linamgogoro na kesi ipo mahakamani ndio wanaokwamisha shuguli zamaendeleo kwenye eneo hilo.
“Tuliahidiwa kujengewa zahanati katika eneo hili ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo karibu na wananchi lakkini imeshindika na kutoka na wacimbaji wachache kuwapeleke wawekezaji hao mahakani kwa ajili ya kudai fidia,” alisema.
Wananchi wachache walikubali kujiunga kwenye kikundi na kuuza eneo kisheria na CANACO waliwalipa Mil200 sasa kuna baadahi walikata kuuza baada ya kuona wenzao wamefanikiwa wanataka  walipwe fidia wakati walikataa kuunga mkono na kuuza maeneo yao,” alliongeza.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger