MUSWADA BINAFSI KUFUTA SHERIA YA MAGAZETI YA 1976
NAPENDA kuujulisha umma kwamba Ijumaa tarehe 4 Oktoba, 2013
nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge muswada binafsi Bungeni kufuta Sheria
ya Magazeti ya mwaka 1976.
Changamoto iliyopo ni Sheria mbadala ya vyombo vya habari baada ya Sheria ya sasa kufutwa. Hata hivyo wad
au wa habari kama
Baraza la Habari Tanzania wameshafanyia kazi suala hili kwa muda mrefu
sana na wana mawazo kuhusu sheria mbadala.
Nimejulishwa
kuwa muswada wa sheria mpya ya habari tayari upo. Kwa hiyo katika
mchakato wa kujadili muswada binafsi wa kufuta sheria ya magazeti ya
mwaka 1976 mabadiliko yanaweza kufanywa ili kutunga sheria mpya.
Hatua
ya kwanza ni kuifuta sheria hii kandamizi ambayo kiukweli tumechukua
muda mrefu sana na baada ya madhara makubwa kufikia hatua ya muswada wa
kuifuta.
Nimeamua kutumia njia za kawaida za kuwasilisha muswada
na kuepuka njia ya dharura ili kujenga mazingira ya wadau wa habari
kushiriki vya kutosha katika mabadiliko yanayotakiwa. Njia ya dharura ni
ya haraka lakini huziba fursa za kupata maoni ya wadau ambao kimsingi
ndio wenye sheria yenyewe haswa.
Hivyo
nimepeleka muswada ili uchapwe kwenye gazeti la Serikali (GN) kwa
mujibu wa kanuni za Bunge, kisha usomwe kwa mara ya kwanza, uende kwa
wadau kwa mjadala na marekebisho na kisha kusomwa kwa mara ya pili na
kupitishwa na Bunge.
Ikumbukwe kuwa juhudi za kufuta sheria hii
ni juhudi za wadau wa tasnia ya habari na ni juhudi walizofanya kwa muda
mrefu sana. Mimi kama Mbunge ninawasilisha tu kwa sababu taratibu zetu
za kuandika sheria zinataka ama Serikali, Kamati ya Bunge au Mbunge
kuwasilisha muswada.
Kwa
muda mrefu tumewaangusha wana habari kwa kutosukuma vya kutosha
mabadiliko waliyokuwa wanayapigania. Hata hivyo, kuna msemo wa kihindi
'asubuhi huanza pale unapoamka'. Sasa tuchukue hatua za kufuta sheria
hii kandamizi.
Zitto Kabwe,Mb
Kigoma Kaskazini
Post a Comment