Tamasha la Fiesta kuendelea Agosti 23 Ijumaa hii mkoani Tabora
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.
TAMASHA la muziki
nchini linalojulikana kama Fiesta 2013, linatatarajiwa kufanyika Agosti 23
mwaka huu mkoani Tabora kwa ajili ya kuwapatia burudani za aina yake.
Linah, mkali wa Bongo FlevaKhufanyika kwa tamasha hilo ni wiki moja tangu ilipozinduliwa rasmi Jumamosi iliyopita ya Agosti 17 mwaka huu katika Uwanja wa Tanganyika, mkoani Kigoma.
AMkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, pichani.
kizungumza jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kampuni ya Clouds Media Group
ambao ndio wandaaji wa Tamasha hilo, Ruge Mutahaba, alisema kuwa wakazi na
wananchi wa Tabora wana kila sababu ya kulisubiri tamasha hilo kwa shangwe.
Ahmad Ally 'Madee'
Alisema kuwa hakuna
tamasha kubwa linalochanganya wasanii wengi kwa pamoja, hivyo wadau wao
wajiandae kupata burudani kabambe kutoka kwao.
“Sisi kama waandaaji
tumejipanga imara kuhakikisha kuwa wasanii wote wanafanya mambo makubwa katika
jukwaa ili kuwapatia vitu vya aina yake wadau na mashabiki wao.
“Hii ni ziara ndefu
inayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, ikiwa na wasanii wengi,
akiwamo Barnabas, Linah, Chege, Mwana FA, AY, Stamina na wengineo,” alisema.
Baada ya kumaliza
ziara zao katika mikoa mbalimbali ya Tanznaia Bara, tamasha hilo litatia nanga
katika jiji la Dar es Salaam, ambapo hushirikisha msanii wa Kimataifa.
Post a Comment